Becky Written Update December 25 2023 Monday Citizen TV
3 min 54 sec25th DECEMBER BECKY UPDATES
PART 1
Imelia aliletwa kwa room yake but alisema hafai kuwa huku. Lexy alimwambia mum, wewe ndio yafaa uwe huku,Junior ndio hafai kuwa huku but mamake alimwambia lets not talk about Junior for a minute. Lexy alimwambia mum, akiwa huku anaeza plan kutuumiza but akaambiwa he is like wonded dog,he can only bark but not bite.
Ghetto kwa Sanchez,aliambia Tito una bahati sana hukufungulia Becky roho angekuacha kwa mataa. Tito akamwambia sikuhizi madem wako hivyo,unadhani ni kupendwa kumbe ni pesa tu anasaka.
Trisha na yeye,lawyer wake alianza kumdai pesa zake,akamwambia si umeona tu tumekua huko na ukashuhudia chenye kilifanyika,ni pesa gani unataka,usinisumbue pia na wewe?? Shantel alirudi na nguo zake zenye alikua amepeana na akauliza Trisha,uko sure hii kastory kako si kauongo?
Trisha akamwambia ningekua nimepata pesa singekua huku ghetto,tulikua very close kusign but Lexy akafika na uncle yake na kila kitu ikachange. Shantel alimwambia usijali, kuna hopes,we have to do something ju mimi sasa nitaambia watu nini na venye nishawaambia mimi nahama ghetto???kuna kitu Trisha alifikiria na akaambia Shantel anarudi,hatujui ametoka anaenda wapi.
Tito ndio kutoka na Sanchez akaambia Tito,hiyo keja umepata,nataka dem wa kwanza unaingiza awe wife. Tito alimwambia usijali,najua chenye nafanya. Punde si punde wakiwa hapo, Shantel akafika akiaccuse Tito kwa kupanga story na Lexy but Tito walimwambia wee usijali chenye kinakuuma ni ati hakuna kitu mtapata huko,Tito hahusiki kwa hii story hata kidogo.
Lexy alimcall Mr Theuri na akamwambia kesho morning,I want to meet the body tomorrow 9am, there is some changes. Mamake alimwambia Lexyyou cant handle everything at the same time what if Junior aamue kukuchallenge kotini? Lexy alimwambia hii inabidi niwe mjanja,ju Junior anaeza iba pesa ahepe,so I have to be keen.
Mamake alimwambia ni sawa but ujue vitu kama hizi hufanya watu hata wanauana so be careful mtoto wangu. Becky na yeye alikuja jikoni,akauliza Moh mbona uliambia Junior tukienda tunaenda na wewe? Moh akamwambia ni ju wee huoni mbele, ama ulikua unataka kutoka na zile mitumba ulikuja nazo?
Junior akitoka huku lazima tutoke na yeye just incase apate share tuko ndani but Becky alimwambia acha kurukia vitu kama bibi ya chief,Junior hatoki huku,bado tuko huku na ujue siko hii hao ju yako. Moh alimwambia ni sawa, uwe hapa ju yangu ama ju ya Jeff ama ju ya Junior,penye uko ndio nitakua.???
PART 2
Junior stress zinamchapa amekuja nyuma ya nyumba kukunywa tu. Becky alikua anamtafuta akamuona kwenye ako akamuuliza babe,unafanya nini solo huku? Whats up? Junior akamwambia Iam just thinking,unajua kifo cha madhe kimeleta mambo mob sana yenye hata sikua nafikiria.
Becky alimwambia babe, usijali,kila kitu kitakua sawa na mimi Iam here for you, lakini Junior akamwambia it's time to get alternative. Becky akamuuliza ipi hiyo? Junior akamwambia there is no relaxing in our family.
Huh! Hii sasa ndio war inaanza yenyewe,hadi Becky alishtuka akarudi nyuma. Junior ameamua ni war sasa na ikibidi watu wakufe. Huku kwa Shantel,ashabuy mayai sita wakule kama breakfast lakini ile njaa Trisha ako nayo alichafua mayai tano within seconds hadi Shantel akamwambia madam,huku si hotel na kama unakula mayai tano itabidi pia uchangie kununua unajua yai moja tu ni 60 bob.???
Siku iliyofuata, Junior alishtukia kuna board meeting Lexy ashaitana na hakua anajua,alikuja akauliza Lexy who do you think you are? Lexy akamwambia Iam Lexy Jabulani the right owner of this wealthy. Junior akamwambia soo hadi umeanza kuongea kiingere, it's not over between us.
Lexy alimwambia ni sawa,unaeza hata enda kotini nitakuanika na pegs ushangae. Wueh! Junor alishikwa na hasira ingine,cheki kutetemeka mikono. Becky alikuja akamuuliza babe ni nini mbaya? Junior akamwambia imagine huyu chokora anasermon board akisema kuna change in management.
Yani Junior ako na hasira ingine hadi anatetemeka but Becky akamwambia please, dont do anything yenye nilikukataza,you kill anyone nakuacha. Junior akamwambia noo,sijasema nataka kuuua mtu mimi na hata sai sijui nifanye nini. Junior hadi alianza kulia akashindwa kuongea kiingereza chake aaongea kibukusu akaambia Becky "axwnceuibags ghfajydyaa busbbj bgsu jgbsgydftukygsh rcdh" sijui kama mtaelewa hapo ju hiyo ni kibukusu???
Lexy ashavaa ready kuondoka na mamake akamwambia unakaa poa sana,just like a CEO. Mamake alimwambia ni sawa but please mum, chenye sitakubaliana na wewe ni kutetea that son of Jezebell. Lexy akakiss mamake na huyoo akaishia.