SULTANA WRITTEN UPDATE NOVEMBER 4 2022
5 min 22 secšššš š
Tunaanzia kijijini kwa Salama,ni baada tu Salama kuwakashifu akina Mwanzele na Babu kwa kumtelekeza na kuacha asaidiwe na JJ,hadi Sada akawaambia chenye Salama anasema ni kweli,kwanza mimi nimeishi kuja huku mnaniangalia na macho,kwanza wewe Zuu,ni mara ngapi nimekuja huku ukinizuia kuingia kwa Salama?
Mnasahau sana kuwa Salama amejitahidi sana kumtunza Sultana na msipojitahidi kulipiza kisasi kwa Major,mimi mwenyewe nitalipiza kisasi kwa Major. Wakashangaa,hadi Zuu akamuuliza utalipizaje kisasi wakati ni kakako? Lakini Sada akawaambia vita vyangu na Major havijaanza sai,ni ya kitambo sana na tangu marehemu babangu Jabali junior aage dunia,Major amechukua mali yote na hapo ndio vita vyangu na Major vilianzia.
Kumbe kwa Major,ndio Dida anafika,mamake akamuuliza ,umetoka wapi wewe na mbona ukalala nje bila kuniambia? Dida akamwambia sikiza mum,last time I checked I wa a grown up na kwa taarifa yako nimetoka kijijini kuombeleza na wenzangu. Fatima akamwambia wenzako si hao wa kijiji,wenzako wako hapa kwa Major. Punde si punde JJ pia akafika na kumnuka alimuona Dida na Kaka wakikumbatiana,akamwambia wewe Dida wewe? wakati nilikuuliza wewe na kaka ulisema hamko kitu kimoja kumbe mnadate. Dida akamuuliza wee unasema nini wewe? JJ akamwambia sikiza,nimekuona wewe na Kaka na inakaa mumedate kwa muda mrefu sana.
Dida akamwambia JJ sikiza,yafaa ufanyiwe soul searching ju nimeona cheti chako na Sultana mshaoana so please spare me your excuses and hunger. Major ndio haamini kwanza alisimama kusikia ati JJ alifanya ndoa na Sultana š¤£š¤£š¤£Fatima pia haamini ju mtu akishafanya ndoa ni hivyo,hainanga rebounce kama githeri.
Turudi kwa Salama,Sada aliambia akina Babu na Mwanzele,nataka kuondoka sasa hivi na nitakaorudi nataka mniambie venye mtakua mumepanga kitu cha kumfanyia Major. Ole wenu nipate bado hamjapanga,nitawawacha.
Haa,tukuje baharini huku,Kokan alimchukua Sultana wakakuja kukaa ufuoni huku huku anamwambia Sultana mimi ndio mwanaume mwenye nakudhamini sana na sidhani kama huyo hata JJ angekufaa,lakini mimi ndio nakufaa. Sultana akamwambia Kokan,sina shida na JJ,shida yangu na JJ ni babake.
Shida ya Kokan hataki kusikia JJ akisemewa ati hana makosaš¤£š¤£kisha sasa Kokan akaambia Sultana mimi naona hivi uende kutalaki JJ ju sasa mbona akufanyie ndoa hospitali? Sultana akamuuliza shida iko wapi hapo? Ndoa ni ndoa iwe hosi ama peponi cha muhimu ni ndoa. Kokan akamwambia apana wewe ni malikia na yafaa ufanye harusi ya kifahari. Sultana aliboeka akamwambia anaenda zake,ju hataki Kokan aseme anything bad kuhusu JJ,ju yeye anajua si JJ amekosana na yeye ni babake ndio hamtaki na maskini wa Mungu hana habari huyu mwenye anachukia ndio babake mzazi.š¤£š¤£
JJ wakti alikuja chumbani mwake,hakujua Dida aliona cheti,alafu akimagine ati mwenye alikua ameoa amemkataa mbele ya watu,manze JJ alianza tu kulia akiwa kwa choo. Dida na yeye pia,ako huku nje analia tu,akikumbuka ati Kaka kuna kadem huwa anaona anakosa kuamini. JJ analia ju ya Sultana,,Dida analia ju ya Kaka,na ati wazazi wa JJ na Dida walitaka JJ amuoe Dida š¤£š¤£š¤£
šššš š
Major baadaye alikuja kumuona JJ. Kwanza akaona ile cert ya ndoa hapo kwa meza akaichukua. JJ bado yuko kwa choo. Major kwanza akakaa chini asome vizuri venye JJ na Sultana wameoana atiš¤£š¤£. Akamuuliza JJ kumbe ni kweli ulifunga ndoa na kile kinyangarika? JJ akamwambia eeh Ndio nilifunga ndoa. Kisha JJ akakuja kutaka kuchukua ile cheti lakini babake alikatalia,akamuuliza,yani umejiona umekua mkubwa hadi unaenda kufanya harusi bila kuambia wazazi sio? JJ akamuuliza nikuambie ili nini ifanyike? Nilimuoa Sultana na najua humpendi hakuna venye ningekuambia. Major alijam akatoka na ile cheti akaenda nayo š¤£š¤£
Fatima na yeye hakuwai taka Major ajue ati Dida na Kaka wanadate,na leo hii Dida amemwaga mtama. Hili jambo linampa kiwewe sana Fatima. Major kukuja,Fatima alimuuliza wamemalizaje na JJ ,lakini badala ya kumjibu,Major alimuita Asiya akamwambia alete kiberiti. Kisha mbele ya Asiya na mbele ya Fatima,Major akateketeza ile cheti ya kuonyesha JJ na Sultana wameoana. JJ kitambo aseme akuje kuangalia alipata cheti chake kinakuliwa na moto kuisha.
Kokan na yeye alimfuata Sultana akamwambia sikiza Sultana humhitaji JJ kuna venye hii hali yako inaeza tibiwa bila hata kufanyiwa upasuaji. Sultana akamsikiza sana Kokan,ju yeye hoja yake iwe JJ ama Kokan chenye anaomba tu ni apate kuona tena.
Kwa Major,alimgeukia Asiya akamuuliza yani harusi inafanywa na huwezi niambia? Asiya akamwambia mimi niliitwa nipike mapochopocho nikadhani pengine ni mualiko wako wa kurudi ndio baadaye nikajua kumbe ni harusi. Major alimwambia Asiya aende,alafu Asiya kuenda tu Fatima akamgeukia Major akamwambia unaona,kumbe ni wewe ndio wamatatizo huku,JJ amekushinda kabisa.
Kumbe Bi Ua na yeye,its now after 3 days anaanza kujihisi,na kitu tu ya kwanza yenye ilikuja kwa akili yake ni ile siku aliambiwa na Asiya kuwa ni kweli alijifungua mtoto wa kike. Kisha akakumbuka venye kulienda hadi akapigwa kofi na Major akaanguka akagonga kichwa chini. Its been 3 days akiwa kwa comma,na leo hii ameanza kujihisi. Ole wake apatikane na Asiya š¤£š¤£
Major na yeye alipigia jamaa fulani mwenye yafaa wakutane akiwa na Fatima,akamwambia rafiki yangu, ilikua tukutane leo lakini nina tatizo mke wangu ni mgonjwa. Lakini Fatima akaona apana,hii ni njama ya Major kumkwepa. Amini usiamini Fatima alikuja akachukua simu ya Major kuangalia akapata ni kweli hakuna mtu mwenye Major amekua akiongea na yeye,ni uongo š¤£š¤£Fatima akamuuliza Major,unataka nikuteketeze mzima sindio? Mbona unaanza kunichezea na unajua inafaa tushughulikie mambo yetu? Major kusikia hivyo,akamuuliza Fatima na wewe,hizi vita za JJ na Dida kuhusu Kaka ulikua unajua sio.na hujai niambia mbona? Ndio maana ulisema Kaka akuje kufanya kazi huku kumbe ulijua ndio umfuatilie sindio? Fatima akajua hapa amaepigwa 10-Nil š¤£š¤£
Tufike chumbani kwa Bi Asiya,yuko pale anapiga pasi manguo fulani hapo hata hana ubaya na mtu. JJ na yeye alitoka kuja huku nje kunywa kawine kiasi. Dida na yeye ndio yule kule nje pia anajipea mawazo yake pole pole na ukiangalia nimekupea majina ya kila mtu na chenye anafanya,kwa nini? kwa sababu kila mtu akiwa kwa shughuli zake,eeh,Bi Ua alipiga nduru ingine kutoka chumbani,mbaya mbovu, Major na Fatima wakashtuka,JJ na Dida wakiwa huku wakashangaa na Asiya akabaki kuduwaa. JJ kusikia mamake anapiga maduru akatoka mbio kuja kuona,Major na yeye kusikia hivyo pia akatoka mbio kuja kuangalia,lakini kama kuna mtu ameshtuka yake yote,ni Bi Asiya ju she didn't see it coming...