Mwongozo Wa Bembea Ya Maisha | KCSE Setbooks Guide
Sun
05
May
24

Mwongozo Wa Bembea Ya Maisha

  1 hr, 51 min, 14 sec  26,852 reads 
BUY NOW Ksh. 200

UTANGULIZI 

 

VIGEZO MUHIMU KATIKA UCHAMBUZI WA TAMTHILIA HII 

 

 

1) Dhamira/ Lengo/ Mintarafu/ Kusudi: Nijambo linalokusudiwa na mwandishi/  lengo kuu la mwandishi.  

2) Maudhui: Jumla ya maswala yanayozungumziwa na mwandishi 

3) Falsafa: Msimamo wa mwandishi kuhusu jambo fulani analoliandikia. 

4) Muwala: Mtiririko wa vitushi/ mawazo katika kazi ya fasihi.  

5) Usuli: Asili /hali inayomzunguka mwandishi na ambayo humchochea kuandika  kazi ya fasihi k.m. usuli wa mwandishi waweza kuwa anazungukwa na jamii  iliyojaa uongozi mbaya / ufisadi ndiyo maana anaandika kuhusu maudhui hayo.  

6) Mandhari: Mahali ambapo wahusika wanatekelezea kazi ya fasihi. K.m. njiani,  shuleni n.k.  

7) Wahusika: Ni viumbe ambao huendeleza mawazo ya mwandishi katika kazi ya  fasihi. Wahusika waweza kuwa binadamu, Wanyama, viumbe halisi au wa  kidhahania (wa kufikirika tu).  

 

 AINA ZA WAHUSIKA KATIKA FASIHI 

 

1) Wahusika wakuu  

• Huchukua nafasi kuu na kukuza kazi ya fasihi.  

• Matendo yote muhimu huwahusu.  

• Dhamira kuu ya mwandishi na falsafa/ msimamo wake hudhihirika  kupitia kwa wahusika wakuu.  

2) Wahusika wadogo  

• Hawana nafasi kubwa.  

• Aghalabu husaidia hadhira kujua zaidi mhusika mkuu na dhamira yake.  

 3) Wahusika wasaidizi  

• Hujenga wahusika wakuu na kukuza maudhui. Aghalabu huja na  kutoweka baada ya muda mfupi.  

• Uainishaji Mwingine wa Wahusika  

4) Wahusika bapa/ Wahusika wa mraba mmoja  

• Huwa hawabadiliki katika hulka/ sifa zao.  

• Mhusika bapa anaweza kuwa na tabia nzuri au hasi kuanzia mwanzo hadi mwisho.  

5) Wahusika duara/ wahusika wa miraba minne  

• Huweza kubadilika kisaikolojia.  

• Huwa na sifa nyingi.  

• Wahusika bapa vielelezo  

• Huwa na tabia za kubadilika ila hujikita katika mtazamo wa mwandishi  na hadhira yake.  

 

• Aghalabu huwa wahusika wakuu na hutumiwa na mwandishi kuendeleza  suala fulani.  

6) Wahusika bapa sugu  

• Wana sifa ya kutobadilika ila huwakilisha walio na tabia potovu katika  jamii. Mhusika bapa sugu anayeweza kuwa mhusika mkuu.  

7) Wahusika hasidi/ wapinzani  

• Hulka zao ni kinyume na mtazamo wa maadili ya jamii.  

• Humpinga mhusika nguli.  

8) Mhusika nguli  

• Ni mhusika anayekinzana na mhusika hasidi kwani anawasilisha maadili  katika kazi ya fasihi. Aghalabu huwa mhusika mkuu au mmoja wa  

wahusika wakuu.  

9) Mhusika shinda  

• Hukuza wahusika wengine kwa kuwa hupelekwa mbele kwa usaidizi wa  wahusika wengine.  

• Huwa chini ya kivuli cha mhusika mkuu.  

• Kupitia kvake ndipo hadhira inapata sifa bayana za wahusika wakuu.  

 

FANI ZA FASIHI/ MITINDO KATIKA FASIHI  

 

Fani ni mbinu ambazo hutumiwa na mwandishi anapoiandika kazi ya fasihi. Fani  hujumuisha:  

a) Mitindo ya lugha: Pia huitwa matumizi ya lugha, mitindo ya lugha, tamathali za  lugha, mbinu za lugha au tamathali za usemi.  

b) Mintindo ya uandishi: Pia huitwa fani za mwandishi, mbinu za uandishi, mbinu  za sanaa au mbinu za usanii.  

 

 

 FA NI ZA LUGHA (TAMATHALI ZA USEMI)  

Ni maneno, sentensi au misemo inayotumiwa kuwasilisha kazi ya fasihi. (Senkoro;  1982). Zinajumuisha:  

1) Takriri/ Uradidi (Repetition): Takriri ni mbinu ya lugha ambayo kwayo  maneno au silabi fulani hurudiwa. Lengo kuu la takriri huwa ni kusisitiza jambo  fulani na kuwavutia wasomaji wawazie jambo hilo.  

2) Maswali Balagha/ Mubalagha (Rhetoric; questions): Haya ni maswali  ambayo hayahitaji majibu. Jibu la swali la balagha huwa akilini mwa  anayeulizwa au anayesoma kazi fulani ya fasihi au huwa tayari analijua. Dhima  ya maswali balagha huwa kutoa mawazo au hisia za ndani za mhusika au  kuweka jambo fulani wazi. Aidha hulenga kusisitiza usemi fulani na kuwasilisha  maudhui.  

3) Methali: Ni kauli fupi ya kimapokeo inayosheheni maana na ujumbe na ambayo  huwa na mizizi katika jamii. Methali huwa na wingi wa hekima na hutumiwa  kupigia mfano. Huwa na maana iliyofumbwa.  

4) Tanakali ya sauti: Ni mbinu ambapo mwandishi huiga tendo fulani na kulipa  matamshi au maandishi.  

 

5) Tashbihi/ Tashbiha/ Mshabaha: Ni ulinganishi/ umithilishaji (usio wa moja  kwa moja) wa kitu na kingine kwa kutumia maneno kama vile: ja, mfano wa,  mithili ya, kama, sawasawa, ungedhani ni... .n.k.  

6) Istiara/ Sitiari: Ni ulinganisho wa kitu na kingine kwa njia ya moja kwa mojae  Ulinganishi huu hufanywa bila kutumia vifananishi.  

7) Nidaa: Ni maneno ambayo hutumiwa kuonyesha hisia za wahusika. Hutumika  kuonyesha hisia za furaha, huzuni, masikitiko, mshangao, mshtuko n.k. 

8) Jazanda: Mwandishi hutaja kitu fulani ambacho kwa kawaida kinaweza  kuonekana kuwa na maana ya kawaida ila kinapochunguzwa zaidi kinaonekana  kuwa na maana ya ndani kuliko ile ya kawaida. Jazanda ni sawa na  kilichositiriwa ndani mwa neno au maneno fulani.  

9) Mdokezo: Mbinu ambapo mhusika mmoja hutaja jambo kisha mwenzake  hulikamilisha au mhusika hutoa wazo/ jambo na kumwacha msomaji  kulikamilisha. Aidha, mdokezo waweza kutokea palipo na upinzani ambapo  mhusika mmoja anaweza akatoa jambo huku mwenzake akilikamilisha atakavyo kwa kumpinga au kumkejeli.  

10)Tabaini: Tabaini ni mbinu ya lugha ambapo mwandishi hutumia maneno  kueleza jambo linaloeleweka waziwazi na msomaji. Ni maelezo ya kina kuhusu j  ambo. Waandishi wengi hutumia takriri/ neno moja ili kuibua tabaini. K.m.  urudiaji wa 'ni' na 'si'. K.v. Walifika watu wa janibu mbalimbali: si wanawake, si  wanaume, si vijana, si watoto — wote walijumuika kumuaga gwiji wa taarabu.  

11)Taniaba: Taniaba yatokana na 'kwa niaba ya'. Kitu/ Jambo hutumiwa  kuwakilisha au kufanya kwa niaba ya kitu/ jambo jingine. K.m. chaki ni taniaba  ya mwalimu; jembe ni taniaba ya mkulima ilhali bunduki ni taniaba ya askari.  

12)Utohozi: Ni mbinu ya kuswahilisha maneno ya lugha nyingine ili yatumike kama ya Kiswahili. K.m. skwota — Squatter, ekisirei X-ray n.k.  

13)Tasfida/ Tauria/ usafidi (Euphemism): Matumizi ya lugha ya adabu/ ya sitara/ ya nidhamu. K.m. Natoka kutabawali (Haja ndogo) badala ya natoka kukojoa;  Alijifungua badala ya alizaa n.k.  

14)Chuku/ Udamisi (Exaggeration/ Hyperbole): Mbinu ya kuongeza chumvi  katika jambo. Mwandishi hueleza jambo kwa namna inayozidi hali halisi ya  jambo hili. K.m. watu waliohudhuria matanga walikuwa wamcjaa pomoni hivi  kwamba hapakuwa na nafasi ya nzi kupita.  

15)Ucheshi/ Kichekesho (Humour): Maneno yanayozua furaha. Msomaji hucheka kutokana na namna mwandishi alivyolieleza jambo.  

16)Kejeli: Pia huitwa dhihaka, kebehi, stihizai au mcheko. Ni kumfanyia mtu, jambo  au kitu dhihaka au kumdunisha mtu au kitu kwa kuonyesha kuwa anachosema  hakina thamani.  

17)Lakabu: Mbinu ya mhusika kupewa au kubandikwa jina na wahusika wengine  au yeye mwenyewe kujibandika jina linaloambatana na sifa zake.  

18)Kuchanganya ndimi (Code mixing): Pia inaitwa kuchanganya lugha,  kuchanganya msimbo au ndimi mseto. Ni mbinu ya kuweka maneno yasiyo ya  Kiswahili katika sentensi ya Kiswahili. K.m. Sina time ya wanawake.  

19)Kubadili msimbo (Code switching): Pia huitwa kuhamisha msimbo,  kuhamisha ndimi au kuhamisha lugha. Ni mbinu ya kuchopeka sentensi ya lugha nyingine katika kifungu cha lugha ya Kiswahili. Utofauti kati ya kuchanganya  ndimi na kubadili ndimi ni kuwa katika kuchanganya ndimi, mwandishi  huchanganya maneno ya Kiswahili na lugha nyingine katika sentensi moja ila  katika kubadili ndimi, sentensi kamilifu ya lugha nyingine hutumika miongoni  mwa sentensi sanifu za Kiswahili.  

20)Ritifaa: Ni mbinu ya kuzungumza na mtu asiyekuwepo au aliyekufa. K.m. Mbona umeamua kuniacha duniani?  

21)Taashira (Symbolism): Ni mbinu ya kutumia lugha ya ishara kuwakilisha  ujumbe fulani.  

22)Majazi: Mwandishi huwapa wahusika majina yanayoambatana na tabia au hulka zao.  

 

FANI ZA UANDISHI (MBINU ZA SANAA)  

 

a) Taharuki (Suspense): Ni mbinu ya kumpa msomaji hamu/ tamaa ya kuendelea  kusoma ili kujua kitakachofanyika baadaye.  

b) Sadfa (Coincidence): Matukio mawili hutokea kwa wakati mmoja bila  kutarajiwa, kupangwa au kukusudiwa.  

c) Barua/ Waraka: Wahusika huandikiana barua. Nyimbo na Mashairi  d) Ndoto/ Njozi/ Ruiya: Maono ya mhusika akiwa amelala.  

e) Uzungumzi nafsia/ Mjadala nafsia: Mhusika hujizungumzia mwenyewe. 

f) Mbinu rejeshi/ Kisengere nyuma: Mwandishi hurejelea mawazo ya msomaji  kwa matukio ya awali hasa kupitia kwa masimulizi.  

g) Kinaya: matukio katika kazi ya fasihi kuwa kinyume na matarajio ya msomaji au hali halisi.  

h) Usemaji kando: Mhusika anayezungumza na wenzake hutafuta faragha labda  kwa kuzungumza bila kumhusisha mwenzake au kupinda kichwa. Mhusika  mmoja anaweza kuwa anamsengenya mwenzake/ au anapinga maoni ya  mhusika mwenzake.  

i) Tadmini: mbinu ya kuchukua mtindo wa lugha au maneno kutoka kwa matini  nyingine na kuweka katika matini fulani. Kwa mfano kuchukua vifungu vya  Biblia kutoka matini ya Biblia na kuyatumia katika tamthilia. K.m. Amini amini  nakwambia. (Kigogo).  

j) Hotuba: mazungumzo ambayo hutolewa kwa hadhira na mtu mmoja.  Mazungumzo haya aghalabu huhusu jambo maalum.  

k) Tashihisi: pia huitwa uhuishi, uhaishaji au uhuishaji. (Personification): Ni  mbinu ya kuvipa vitu visivyo na uhai sifa za au kutenda kama kitu kilicho na  uhai.  

l) Utabiri/ ubashiri: Ni mbinu ya kueleza kuhusu mambo ambayo yatatokea  baadaye.  

m) Mhusika ndani ya mhusika: mhusika fulani huiga maneno au matendo ya  mhusika mwingine na kutenda kama yeye.  

n) Mbinu maarifa mtambuka: Msanii kuingiza maarifa ya taaluma (uwanja  mwingine wa kitaaluma) katika kazi yake.  

 

o) Taswira: Ni mbinu ya mwandishi kutoa maelelzo kuhusu jambo au mtu  yanayojenga picha (Mawazo ya akilini) ya jambo au mtu huyo hivi kwamba  msomaji huona picha kamili ya kitu/ jambo au mahali hapo. Dhima ya taswira  huwa kumwezesha msomaji aelewe zaidi jambo husika.  

 Aina za taswira  

 

i) Taswira muonjo/ mwonjo: msanii anaweza kutueleza namna chakula  kilionjwa hadi msomaji akataka adondokwe na mate.  

ii) Taswira oni: msanii hutoa maelezo hadi msomaji akaona picha ya kitu/  jambo fulani mawazoni.  

iii) Taswira hisishi: msanii anaweza kueleza hisia za mhusika fulani kama  furaha, majonzi n.k.  

iv) Taswira msanii anaeleza jinsi ambavyo alisikia jambofulani kwa nakini. v) Taswira mnuso: msanii anaeleza mambo kuhusu harufu anayoingiamua  kupitia pua,  

vi) Taswira mguso; msanii anaeleza alivyohisi kwa mguso. 

Katika maandalizi ya kuukabili mtihani(kuyajibu maswali), ni vyema mwanfunzi  azingatie mambo yaliyo hapa chini ili aweze kuyamudu maswali yatakayotokana na  kazi anazozishughulikia.  

Isome kazi mara kadhaa ili kuifahamu kazi husika ndani nje. Kuisoma kazi mara  moja na kujidanganya kuwa umeielewa si vyema. Hakikisha kuwa umeyafahamu  mambo yote muhimu katika kazi ya fasihi na kuyahifadhi katika ncha za kucha  zako(yakumbuke kwa urahisi).  

Wakati wa kusoma kazi hizi, hakikisha kuwa una penseli ili kupiga nmstari mambo yote muhimu k.m mbinu za lugha, wahusika, nk. Vile vile hakikisha unaongeza  pembeni mambo yote muhimu yanayojitokeza unapoendelea kutagusana na kazi.  

Fahamu kuwa sehemu hizi tatu hutahiniwa. Kila sehemu hubeba alama 20.  Wakati wa kuyajibu maswali ya mtihani, mwanafunzi achague maswali ambayo  anayamudu vilivyo ili kujizolea alama nyingi zaidi.  

Mwanafunzi vilevile asipuuze mambo mawili yafuatayo wakati wa kuukabili  mtihani;  

Hati  

Hati ni mwandiko yaani namna mtu anavyoandika. Hati huwa kigezo muhimu sana  katika mtihani. Ni vyema mwanafunzi aandike kwa hati inayosomeka vyema kwa  urahisi. Ukiandika kwa hati 'nadhifu' mtahini hatatatizika kuisoma kazi yako wala  kutumia muda mwingi akijaribu kuisoma kazi yako. Ni vyema uzingatie namna  ulivyofundishwa kuandika herufi katika chekechea. Herufi zingine zisizoeleweka  ambazo wanafunzi huweza kuandika si za Kiswahili na hazina maana katika Kiswahili,  ziepuke.  

 

Makosa ya kisarufi  

 

Japo makosa haya hayaadhibiwi katika karatasi hii ya 102/3, ni vyema mwanafunzi  ayaepuke mno. Makosa haya yakikithiri yanaweza kuupotosha usahihi wa jibu kiasi cha mtahini kuamua kukuadhibu na bila shaka utakuwa umepoteza alama. Makosa mengine ya kuingiza herufi zisizo za Kiswahili kama vile 'X', 'C' nek katika kuendeleza maneno ya Kiswahili visivyo pia hupotosha umantiki na usahihi wa jawabu.

  

JINSI YA KUKABILIANA NA MASWALI  

 

Baada ya kuisoma kazi yoyote ile ya Fasihi Andishi, mtihani hufuata. Kwa hivyo ni  vyema kujihama na mbinu za kuyakabili maswali.  

Mwanzo, fanya utafiti zaidi kuhusu usuli wa kazi unayasoma, falsafa au mtazamo wa  mwandishi n.k. Ihakiki kazi yenyewe kwa undani ili kuhakikisha umeelewa maudhui,  wahusika, matumizi ya lugha, mandhari na fani nyingine zilizomo. Ili kujitayarisha  kuyajibu maswali katika mtihani wa fasihi, ni muhimu kuelewa kuhusu Uteuzi wa  maswali. 

 

Tatizo kubwa linalowakumba watahiniwa katika mtihani wa fasihi ni uteuzi wa  maswali. Kati ya maswali saba yanayotahiniwa, mtahiniwa anatakiwa kuchagua  maswali manne.  

 

Ikumbukwe kuwa Riwaya, Tamthilia na Hadithi Fupi ni kati ya maswali haya saba  yaliyotahiniwa. Kwa hivyo, hakikisha unaangazia yafuatayo katika sehemu hii;  

a) Uzito wa swali - kadiria uzito wa maswali kwa kuangalia alama zinazotolewa  kando ya swali. Swali la alama 20 linahitaji hoja kumi zilizojadiliwa vyema.  b) Hoja za kutosha. Usivamie maswali bila kuwa na hakika kama una hoja za  kutosha kuyajibu kwani huenda utakwama katikati. Kama swali lina alama 20,  hakikisha una hoja kumi zenye uzito.  

c) Kulielewa swali - Elewa swali na kuangalia kama lina vijisehemu.  Iwapovijisehemuvyake vinahusiana na sehemu ya kwanza, jihadhari usije  ukakosa kuonyesha uhusiano huo. chukua muda kuchagua swali, kwa  

d) Kuchagua swali kuandika vidokezo vya kulijibia kando ya swali lenyewe. Ni  vyema kuchagua swali ambalo utapata zaidi ya alama 15.  

 

e) Kuyaelewa maagizo kumbuka kuwa, maswali hutungwa ili kujibiwa kwa  kuzingatia maagizo. Unapaswa kulichukua jukumu la kusoma, kuelewa na  kufuata maagizo. Kwa mfano, kuna maswali ambayo ni ya lazima, na maswali ya  kuchagua. Kadhalika, maagizo hufafanua jinsi ya kuchagua maswali, k.v. jibu  swali la tatu au la nne. Usijibu maswali mawili kutoka kitabu kimoja na  kadhalika. 

 

f) Kuuelewa msamiati wa swali -- pamoja na maagizo, zingatia pia msamiati wa  swali. Kwa mfano unapoambiwa - taja na ueleze, lazima uelewe kwamba,  mtahini katika mwongozo wake wa kusahihisha, atakuwa na tuzo yakutaja  mambo manne, kwa mfano, aghalabu utakuta neno manne limekolezwa wino.  

 

Hakikisha kuwa una hoja nne zilizo sahihi. Iwapo utaandika hoja zaidi ya nne,  mtahini atachukua hoja nne za mwanzo tu, hata kama umezikosea na hatatuza  hoja zinazofuata japo zitakuwa sahihi. 

 

 

AINA ZA MASWALI  

Kuna aina mbalimbali za maswali. Kila moja yazo huwa na mahitaji yake. Kuna aina  mbili za maswali yanayotokea katika tamthilia na vitabu vingine viteule: maswali ya  insha na maswali ya muktadha wa dondoo.  

Maswali ya insha huandikwa kwa nathari. Jiepushe na kudondoa hoja au  kuziorodhesha. Wakati ambapo maswali ya insha yanahitaji majibu ya kina na hoja  zilizofafanuliwa kikamilifu, yale ya muktadha yanamhitaji mtahiniwa awe ameielewa  tamthilia kwa undani ili aweze kufafanua muktadha wa dondoo alilopewa bila  kukatizika. Hii itamwezesha kulitambua dondoo lilikotolewa kwa urahisi. 

 

Katika kufafanua muktadha wa dondoo, mtahiniwa anahitajika kujibu maswali  manne kwa usahihi:  

1. Nani anaongea?  

2. Anaongea aongea na nani?  

3. Wakiwa wapi au katika hali gani?  

4. wanaongea kuhusu jambo gani?  

 

JALADA LA BEMBEA YA MAISHA 

Jalada ni sehemu iliyoko juu ya kitabu Huwa ni mambo yaliyo muhtasari wa  kile msomaji anataraji ndani. Jalada huwa kuwili yaani, jalada la mbele na la  nyuma. Kunavyo vipengele muhimu hasa rangi za michoro na maandishi. 

Jalada la tamthilia ya Bembea ya Maisha limechorwa mwanamume na  wanawake wawili wakiwa wamekumbatiana. Watu hao wameketi kwenye  bembea. Mwanamume huyo anawakilisha Yona na wanawake hao  wanawakilisha Sara na Neema.  

Wote wanaonekana kufunga macho kuonyesha wako katika hali ya utulivu wa  moyo. Hali hii ya kukumbatiana inadhihirisha kwamba kuna upatanisho wa  familia ambayo ilikuwa imeyumbishwa na bembea ya maisha.  

 

ANWANI YA TAMTHILIA  

❖ Bembea ni kifaa kama vile ubao, kamba au chuma inayoninWinia baina ya  chuma au mti ambacho hutumiwa kuchezea aghalabu na watoto.  

❖ Bembea huenda juu na chini au mbele na nyuma. Ili mtoto aweze kucheza na  bembea, wakati mwingine kuna anayeisukuma bembea hiyo.  

❖ Bembea ya maisha ni namna maisha yanavyoendesha watu.  

 

❖ Katika tamthilia hii, maisha yamesawiriwa kama bembea. Kuna wakati maisha  ya wahusika yamejawa na furaha na mafanikio tele na kuna wakati maisha ya  wahusika yanaenda chini, wanakumbwa na shida na matatizo.  

Kwa mfano:  

Maisha ya familia ya Sara na Yona yanaleta taswira ya bembea. Mwanzoni, ndoa  ya Sara na Yona inaonekana yenye furaha. Hii ina maana kuwa, kama bembea  inavyokuwa juu, maisha yao yalikuwa yenye mafanikio na furaha. Maisha yao  yanaingiwa na dosari wakati wawili hao wanakosa mtoto baada ya kipindi kirefu katika ndoa. Zaidi ya hayo, wanajaliwa na watoto wa kike watatu. Hawajaliwi na  mtoto wa kiume, kinyume na matarajio ya jamii. Wanachekwa, wanasutwa na  kukejeliwa.  

 

Bembea ya maisha yao inarudi chini. Sara anaanza kuchapwa kichapo cha mbwa  na bwana yake Yona. Yona anaidharau familia yake na kuingilia ulevi, ulevi  uliomfanya kupigwa kalamu kazini. Sara anasema, japo kuna wakati maisha  yanabwagwa na bembea ya maisha, lazima maisha hayo yaendelee. Hata kama  kamba, chuma au minyororo ya maisha inakatika, hawana budi kujiinua na  kuendelea na maisha (uk. 20-21). Hivyo basi Sara anasimama na familia yake  kidete akifahamu kuna siku atafanikiwa na maisha yao yatakuwa mema tena. 

 

Maisha ya familia ya Yona yanabadilika kutoka kuwa maisha ya kukosa mahitaji  ya kiuchumi. Bembea yao ya maisha ilionekana kuwachini. Baada ya Neema  kufanikiwa na kupata kazi, bembea ya maisha yao inakuwa juu. Wanafanikiwa  kujengewa nyumba, wanapata wafanyakazi wa kuwasaidia nyumbani na hata  kuwa na jiko la gesi la kupikia.  

Bembea ya maisha ya Neema inaonekana kusukumwa na Bunju mumewe.  Kwanza Bunju alimsaidia Neema alipokuwa amepata ajali. Bunju alimtumia flying doctors ili aweze kupata matibabu zaidi (uk. 41).  

Bunju anasaidia kuisukuma bembea ya maisha ya Neema kwa kumsaidia  kuwasomesha dada zake. Vilevile, anamsaidia kuwajengea wazazi wa Neema  nyumba.  

 

Maradhi ya Sara yanaifanya bembea ya maisha ya Sara kuwa kama iliyokatika na kuwa chini. Sara anakosa matumaini ya kuishi na kutamani kufa.  

 

Bembea ya maisha ya mjini huwa juu kutokana na maendeleo. Kuna maendeleo  ya barabara, magari mengi, majengo mengi na hata sekta ya matibabu  imeimarishwa.  

 

Watu mjini wanapokea matibabu ya hali ya juu ilhali, bembea ya maisha ya  kijijini huwa chini kwa sababu ya kukosa maendeleo hasa katika sekta ya  matibabu na barabara nzuri. Sekta ya matibabu ya kijijini inamfanya Neema  kumtafutia mamake hospitali ya mjini sababu zile za kijijini hazimpi mtu  matumaini ya kutoka akiwa mzima ilhali za mjini zinampa mgonjwa matumaini  ya kutoka akiwa buheri wa afya. 

 

 

Dhamira ya mwandishi  

 

Dhamira huelezwa kama lengo au shabaha ya mwandishi wa kazi ya fasihi.  Mwandishi wa tamthilia ya Bembea ya Maisha anadhamiria:  

🙓 kuonyesha masaibu ya pombe katika maisha ya familia  

🙓 kuonyesha kuwa ili kujenga jamii mpya, mapinduzi ni muhimu na ni lazima  wanajamii wajitolee kupinga tamaduni zisizo na umuhimu wowote katika  maisha ya wanajamii  

🙓 kutuonyesha kuwa watoto wa jinsia zote ni sawa na hawafai  

🙓 kutenganishwa kwa mila na tamaduni za jamii  

🙓 kutuonyesha kuwa hakuna lililo na mwanzo lisilokuwa na mwisho.  

 

MTIRIRIKO WA MAONYESHO  

 

Sehemu I  

Onyesho I  

⮚ Nyumbani kwa Sara, Sara ameketi kwenye kochi baada ya kumeza vidonge vya  dawa kwa sababu ya maradhi yanayomsumbua. Yona anayeonekana mchovu na  mwenye kukinai anaingia kwa nyumba.  

⮚ Onyesho linaanza kwa kuonyeshwa namna Yona asivyofurahia hali katika  nyumba yake. Analalamikia Sara kuwa hajamwandalia chakula. Yona  hababaishwi na hali ya Sara ya ugonjwa, haja yake ni chumba kivuke moshi. Sara anamweleza namna mwili wake ulivyo, hapo mazungumzo kuhusu mwana wao,  Neema, yanaanza. Yona anatoa wazo lake kwa Sara amwite bintiye aje ampeleke  hospitalini. Sara anakataa wazo hilo kwa kukiri kuwa bintiye ana familia yake  ambayo anafaa kuishughulikia.  

⮚ Maoni ya Sara yanazua mgogoro baina yake na Yona kuhusiana na mtoto wao  Neema. Yona anashikilia kuwa ni jukumu la bintiye kuwajibikia matibabu ya  mamake, naye Sara anashikilia kuwa bintiye ana majukumu ya kwake na tayari  amewafanyia mengi, kwa hivyo, awachwe apumzike.  

⮚ Mgogoro huu unasawazishwa onyesho linapoelekea kuisha. Sara na Yona  wanakubaliana kuwa wanafaa kumpa binti yao baraka zao.  

⮚ Onyesho linamalizika kwa kuonyeshwa Yona akirejelea suala la chakula. Sara  anamweleza asubiri kwa kuwa amempelekea Dina salamu aje awafanyie  chochote.

  

Masuala makuu 

⮚ Onyesho hili linakunjua jamvi la mjadala kuhusiana na majukumu ya watoto kwa wazazi wao. Inabainika kuwa katika jamii nyingi watoto wa kiume ndio  wanaotarajiwa kuwatunza wazazi wanapozeeka.  

⮚ Inachukuliwa kuwa watoto wa kike walioolewa wanapaswa kupewa fursa ya  kushugulikia jamii za kule walikoolewa. Ingawa Neema ni mtoto wa kike,  anaonekana kuyamudu majukumu yake kama ambavyo mtoto wa kiume  angaliweza kuyamudu. Msemo wa 'kutoa ni moyo usambe ni utajiri'  

 

unadhihirishwa na matendo ya Neema. Mazungumzo baina ya Sara na Yona  yanadhihirisha kuwa hata ajira za kiwango cha chini kama zile za kufanya kazi  shambani na nyumbani pia huwa na changamoto zake. Baadhi ya waajiriwa  huwaibia waajiri wao huku wengine wakidhihirisha hali za uvivu na kushindwa  kutekeleza wajibu wao kama inavyotarajiwa.  

Onyesho Il  

✔ Onyesho hili linatukia nyumbani kwa Dina. Kiwa alikuwa amefika nyumbani  kumjulia hali mama yake.  

✔ Onyesho hili linaanza kwa kuonyeshwa namna Kiwa anavyogusagusa chakula na kudai ametosheka. Katika harakati ya mazungumzo juu ya chakula, Dina na Siwa  wanajikuta wakizungumza kuhusu familia ya Yona na Sara. Dina anamweleza  mwanawe Kiwa namna familia hiyo ilivyodunishwa na wanajamii kwa kukaa  muda mrefu bila kujaliwa na watoto na hata baada ya kufanikiwa na watoto  wasichana, jamii iliendelea kuwasuta na kuwakejeli kwa kuwa hawakujaliwa na  mtoto wa kiume atakayerithi fimbo ya baba yake. Kusemwa huku na wanajamii  kunasababisha Yona kuingia katika ulevi, ulevi ambao unamsukuma kumdharau  na kumchapa bibi yake kichapo cha mbwa.  

✔ Onyesho linaisha kwa kuonyeshwa Dina akimuaga Kiwa ili aweze kwenda  kumsaidia Sara katika harakati ya mapishi kwa kuwa Sara alikuwa anaugua.  

Masuala makuu  

⮚ Onyesho hili linamulika masuala matatu muhimu. Taasubi ya kiume na mila  potovu, ukosefu wa ufahamu kuhusu chanzo cha jinsia ya watoto na umuhimu  wa bidii maishani. Kulingana na somo la Biolojia, chembechembe za kromosomu zinazofanya uamuzi wa jinsia ya mtoto hutokana na wazazi wa kiume ambao  wamebeba kromosomu aina ya Y isababishayo kuzaliwa kwa mtoto wa kiume.  Mwanamke hana uamuzi kuhusiana na jambo hili. Hali ya kuwafedhehesha na  kuwanyanyasa wanawake kutokana na kuzaliwa kwa watoto wa kiume halina  msingi wowote. Tatizo hili linatokana na ubabe dume na taasubi ya kiume. Hali  hii inatiliwa mbolea na utamaduni potovu wa jamii kutaka kumrithisha mtoto  wa kiume na kumkandamiza mtoto wa kike. Suala la bidii maishani linajitokeza  kama kiungo muhimu cha ujenzi wa maisha.  

⮚ Dina anajitolea kuwasaidia Sara na Yona katika kazi za nyumbani kutokana na  hali mbaya ya afya ya rafikiye Sara. Tendo hili linadhihirisha udugu na ujirani  mwema.  

Onyesho III 

⮚ Onyesho hili linatokea nyumbani kwa Sara, jikoni. Dina yupo katika harakati ya  mapishi naye Sara amejikunyata kwenye kibao. Mchuzi u tayari. Sara  anamshukuru Dina kwa kufika kumsaidia. Dina anapokea shukrani na kumpa  Sara maneno ya kumtia nguvu. Dina anamweleza Sara kuwa kila kitu hufanyika  

 

kwa mpango wa Manani. Anamweleza atazame faraja ilivyovuka kwake kwa vile  watoto wake wamefaulu maishani. Anampa matumaini kwamba atapona kwa  kuwa hospitali ambayo Neema anampeleka ina watalaamu.  

⮚ Mazungumzo ya matumaini yanaendelea kunoga huku Dina akiendelea na  mapishi. Dina anauliza Sara alikokwenda Yona na hapo mazungumzo kuhusu  mwanamume na utamaduni yanazuka.  

⮚ Tunaelezwa namna utamadumi ulivyowajenga wanaume kama watu wasiofaa  kuingia jikoni.  

⮚ Onyesho hili linatimia Sara akimweleza Dina kuhusu mipango iliyopangwa na  Neema kuhusu namna atakavyorudi kliniki kupata matibabu.  

Masuala makuu 

Katika onyesho hili inadhihirika wazi kwamba taasubi ya kiume imemtawala  Yona na kumfanya kutoona hali ya unyonge wa mkewe.  

Inamlazimu Sara kuomba usaidizi kwa jirani ndipo waandaliwe chakula ilhali ni  kazi ambayo Yona angeifanya bila malalamishi na kuficha siri ya familia yake.  Suala la wanaume kutosaidia katika shughuli za nyumbani hutokana na mila na  desturi ambazo zinamdhalilisha mwanamke. Mwanamume anapomsaidia  mkewe jikoni huona ni kama kwamba hadhi yake imeshushwa.  

La kutia moyo ni kwamba, ingawa jamii inamdhalilisha mwanamke, ni dhahiri  kuwa mwanamke wa sasa amejizatiti na kujiinua na kufikia kiwango cha  kutajika. Neema anakuwa mfano mzuri katika jamii kwa kuyabeba majukumu  yake binafsi na yale ya nyumbani alikotoka.  

Anahakikisha mama yake anatibiwa na kumfanya Yona amuonee fahari si tu  kama msaidizi bali nguzo muhimu ya kutegemewa hata ingawa ni mtoto wa  kike, tena aliyeolewa.  

Umuhimu wa ujirani mwema pia unazungumziwa. Dina anajitokeza kuwa jirani  na rafiki wa kutegemewa wa Sara. Ni wazi kuwa Sara na Yona wanaishi vizuri na majirani wao.  

 SEHEMU I I 

Onyesho I  

⮚ Nyumbani kwa Neema, Neema na mamake wameketi ukumbini wanazungumza.  Sara amefika mjini kwa ajili ya matibabu na amechoka kutokana na safari ndefu.  ⮚ Neema anashangazwa na kuchelewa kwa Lemi kutoka shuleni. Anakumbushwa  na Bela kuwa Lemi anajiandaa kwa hafla itakayofanyika shuleni na ambayo  Neema ameisahau kwa sababu ya  

⮚ Neema anamsaili mamake kuhusu sababu za vurumai za mara kwa mara za  Yona. Sara anamweleza kuwa vurumai hizo zilizomsababishia maradhi ya moyo  zilitokana na ulevi; kwamba Yona alitaka amzalie mtoto wa kiume. Jamii nayo  ilimsukuma Yona aoe mke mwingine ili azaliwe mtoto wa kiume ambaye Sara  hakufanikiwa kupata. Yona aliposhindwa kuhimili shinikizo hizo aliingia katika ulevi hadi akafutwa kazi. Mbali na haya, Sara anamtetea Yona kwa hali na mali  kuhusu tabia yake ya ulevi na vurumai.  

⮚ Ni katika onyesho hili tunapomwona Neema akilalamika kuhusu Bunju,  mumewe. Kulingana na Neema, Bunju anaonekana mgumu wa pesa. Anajitetea  kwamba amebanwa na mahitaji mengi ambayo hayamwachi na fedha za ziada.  ⮚ Tathmini  

⮚ Kupitia kwa mazungumzo haya, masuala kadhaa yanajitokeza yakiwemo  maeneo ya mashambani yaliyopuuzwa kimaendeleo, bidii maishani, taasubi ya  kiume pamoja na athari za uraibu wa pombe. Usemi 'mrina haogopi nyuki,'(uk.  18) unaotumiwa na Sara unaelezea bidii inayohitajika ili mtu afaulu maishani.  Kwamba, sharti mtu akabiliane na magumu anayokumbana nayo. Sara  anayasema haya anapogundua kuwa Lemi ana kazi nyingi za kufanya huko  shuleni. Kwa sababu ya kazi hizo, inakuwa vigumu kwa Sara kuonana na mjukuu wake.  

⮚ Suala la uwajibikaji miongoni mwa wanasiasa linajitokeza pia. Suala hili  linaangaziwa kupitia usafiri unavyotatizwa na miundo misingi duni katika  sehemu za vijijini.  

⮚ Inabainikakwambayonaanajitokomezaulevinikutokananamsukumo wa  wanajamii kwa kukosa kuzaa mtoto wa kiume. Huu ni utamaduni uliopitwa na  wakati. Pombe inakuwa kimbilio la kumsahaulisha malengo aliyoshindwa  kuyafikia. Sara anasisitiza kwamba wazazi wana wajibu wa kumlea mtoto wa  jinsia yoyote ile bila ubaguzi.  

Onyesho Il  

🙓 Onyesho hili linafanyika nyumbani kwa Neema akiwa na Bela, mfanyakazi wake.  Kupitia mazungumzo yao inabainika kwamba maisha ya leo yana changamoto  nyingi kiasi kwamba wazazi hawatangamani na watoto wao jinsi  

inavyotakikana. Hali hii inaonekana kuwakera wazazi.  

🙓 Suala la shughuli nyingi kazini linaonekana kuhitilafiana na shughuli ya malezi.  Katika sehemu hii inabainika kuwa Neema haonani na Lemi kwa sababu kila  afikapo nyumbani mtoto huwa amelala.  

🙓 Suala la mila pia linaibuka. Wazazi wa Sara hawawezi kulala kwa mtoto wao  aliyeolewa. Neema analizungumzia jambo hili kwa mshangao. Hili ni jambo la  kutatiza kwa sababu mara kwa mara mamake Neema huenda mjini kwa  shughuli za matibabu na huwa anahitaji mahali pa kulala.  

🙓 Isingekuwa kwamba Asna anaishi mjini na kwamba anaweza kumuauni  mamake, basi ingempasa Neema kumkodishia chumba mamake, jambo ambalo  Kiafrika ni makosa. Suala la utandawazi linajitokeza na ni dhahiri kwamba  baadhi ya mila zimepitwa na wakati na zinapaswa kutupiliwa mbali kama Bela  anavyoeleza:  

🙓 Hayo ni ya kale...na ya kale hayanuki. Wengi hawafuati tena mila hizo.  Walimwengu sasa wanavaa sare moja (uk. 24). Kauli hii inaonyesha namna  

 

mabadiliko ya kijamii yamefanya baadhi ya mielekeo ya kitamaduni kupuuziliwa mbali.  

Masuala makuu  

Sehemu hii inadhihirisha jinsi hali za maisha ya kisasa zinavyowatatiza wanajamii.  Wanalazimika kufanya kazi mchana kutwa ili kujikimu na kuzifaa familia zao. Matokeo  ni kwamba hawapati nafasi ya kutangamana na familia zao ipasavyo. Ni bayana  kwamba bado wanajamii wamefungwa na mila ambazo kwa hakika ni vigumu kuzitii  kwa sababu ya maisha ya kisasa. Mfano mzuri ni miko inayowazuia wakwe kutolala  katika makaazi ya wana wakwe zao.  

Onyesho Ill  

🙓 Katika onyesho hili Bunju yuko tayari kuondoka kwenda kazini asubuhi.  Mazungumzo na mkewe Neema yanahusu matokeo ya mitihani ya Lemi, mtoto  wao. Huku Neema akionekana kuridhishwa na matokeo hayo Bunju anamtaka  Lemi kujitahidi zaidi ili apate matokeo ya kuridhisha zaidi. Mgogoro baina ya  wazazi kuhusu masomo ya watoto wao unajitokeza. Hali ya Neema na Bunju  kutokubaliana kuhusu bidii ya mtoto wao inaweza kuzua msukosuko.  

🙓 Neema anapomwelezea Bunju kuwa mamake tayari ameshafika mjini kwa  matibabu, anakataa kutoa pesa za kusaidia matibabu hayo. Bunju anadai kuwa  ana majukumu mengi. Kwamba anagharamia mahitaji yote ya nyumbani,  yakiwemo karo ya shule, kodi ya nyumba na amemnunulia Neema gari.  Anamtaka Neema awajibike kwa sababu amemruhusu kutumia mshahara wake  kwa mahitaji ya familia yake.  

🙓 Bunju anasisitizia ile dhana ya kutomruhusu mama mkwe kulala nyumbani  kwao. Mila na desturi hizo zinamkera Neema sana. Kwa Neema, hizo ni mila na  desturi zilizopitwa na wakati.  

Tathmini  

✔ Onyesho hili linazungumzia mambo muhimu ya kifamilia, hasa malezi na elimu.  Neema anaridhishwa na matokeo ya mwanawe, ila Bunju anamtaka Lemi  aongeze bidii masomoni. Hayo yakijiri, inaonekana kana kwamba ni Neema  pekee anayejitahidi kushughulikia matakwa ya Lemi shuleni. Bunju analipa karo  na kutekeleza majukumu mengine ila kazi yake imembana hadi hana muda wa  kutangamana na familia yake ipasavyo. Mfumo wa uchumi umewagandamiza  raia na kuwalazimisha kufanya kazi masaa mengi kupindukia.  

✔ Mfumo wa elimu unawapa watoto shinikizo la kujibidiisha zaidi masomoni,  jambo ambalo linaweza kusababisha msukumo wa kiakili miongoni mwa  watoto. Ni bora wazazi wakiwa na msimamo mmoja kuhusu masuala  yanayohusu elimu ya watoto wao.  

✔ Mchango wa mwanamke katika ndoa unamulikwa. Bunju analipa kodi ya  nyumba, karo na hata kamnunulia mkewe gari. Je, mchango wa mkewe katika  

majukumu ya kifamilia ni upi? Ni muhimu mwanamke anayefanya kazi  kuwekeza kiwango fulani cha pato lake katika mali ya familia ili kupata heshima  na pia kama njia mojawapo ya kujifunza kuimudu familia ikiwa ataondokewa na  mumewe mapema.  

Onyesho IV  

🕮 Mjini, nyumbani kwa Asna. Asna anamwandalia mamake kiamshakinywa. Mama  mtu anashangaa mbona bintiye anaishi katika chumba kidogo. Bintiye anajitetea  kuwa chumba hicho kiko katika mtaa wa kifahari na anakifurahia. Sara  analinganisha maisha ya mjini na ya kijijini na kuona kuwa yale ya mjini yanaudhi,  afadhali ya kijijini.  

🕮 Anasema kwamba, watu wa mjini wako mbioni kila wakati na mapato yao ni haba.  Asna hakubaliani na mamake; kwake, kiwango chake cha elimu hakimruhusu  kwenda kukaa kijijini.  

🕮 Sara anamsihi Asna aolewe amletee mjukuu. Asna hakubaliani na jambo hilo.  Kulingana na Asna, ndoa ina matatizo mengi kama yale anayopitia Neema, dada  yake, ambaye ingawa amesoma na kupata shahada mbili, hazimsaidii kupigana na  msimamo wa kitamaduni alionao Bunju, mumewe. Badala ya kupigania mabadiliko  ya msimamo wa Bunju, Neema anaonekana kuukubali kwa sababu ya uhuru wa  matumizi ya mshahara wake aliopewa na Bunju.  

🕮 Utepetevu kazini unazungumziwa kupitia madaktari na utendakazi wao. Baadhi ya  madaktari daima wako mbioni kutoka hospitali moja hadi nyingine ili kuchuma hela za ziada bila kuwazingatia wagonjwa wao kikamilifu.  

Masuala makuu 

🕕 Kuna mambo muhimu yanayojadiliwa katika onyesho hili. Jambo la kwanza ni  hadhi. Ile hali ya kutaka kuishi sehemu za kifahari hata ingawa pato ni dogo.  Asna anaishi maeneo ya juu ingawa mazingira ya nyumba yake ni duni.  Anajikakamua kulipa kodi ya juu ya nyumba bila kujali mazingira anamoishi.  

🕕 Jambo la pili linaakisi athari za elimu ya juu dhidi ya mila na desturi za Kiafrika.  Inasahaulika kwamba,elimu pekee bila uelewa haiwezi kubadilisha dhana na  fikra za kitamaduni. Bunju ana elimu lakini elimu yake haijamtoa katika mila na  desturi za jamii yake. Neema ana elimu lakini haimsaidii kuelewa chanzo cha  mila na desturi za Bunju. Jambo la tatu ni kutosheka kwa mwanamke. Neema  anaonekana kutosheka na hali ya mumewe ya kumruhusu kutumia pesa zake  atakavyo. Hafikirii kuwa huenda ikawa ni mtego. Mara nyingi mwanamke  anapopata uhuru wa aina hii, huweza kubugikwa na akili asiweze kufikiria  kuwekeza kwa ajili ya maisha ya baadaye. Kisha mambo yanapoharibika  hujikuta hana lolote la kutegemea.  

Sehemu III 

Onyesho I  



 

🙓 Nyumbani kwa Neema na Bunju. Neema yuko nyumbani anafanya usafi.  Anafikiria jinsi ugonjwa wa mamake ulivyomfanya fukara. Bunju anapoingia  chumbani, Neema hamsikii, anashtuka. Kwa mara nyingine, anakataa kumsaidia  Neema kugharamia ugonjwa wa mamake.  

🙓 Anasema kwamba anafanya majukumu yote ya pale nyumbani na haoni ni kwa  nini Neema hawezi kuupangia mshahara wake ili uweze  

🙓 kuyakidhi mahitaji yake. Neema anahuzunishwa na msimano wa Bunju lakini pia anakumbuka maneno ya mamake kuwa Bunju ni zawadi kwake, jambo ambalo  linampa heri kidogo.  

Masula makuu  

🙓 Onyesho hili linampa msomaji au mtazamaji nafasi ya kuelewa mahusiano katika taasisi ya ndoa. Wanandoa hao wawili wanashikana mkono kuendeleza maslahi  ya jamii yao. Mume anaheshimu rai ya mkewe ya kutumia hela zake  kushughulikia wazazi wake ambao ni wahitaji.  

🙓 Mama ni mgonjwa na baba yake amepoteza ajira. Tofauti ya matumizi ya pesa  kati ya mwanamke na mwanamume yanajitokeza. Mwanamume anajenga na  mwanamke anapamba. Mambo yanapoharibika, mwanamke huachwa bila  makao kwa sababu ya dhana kuwa hakuwekeza katika  

🙓 ujenzi wa nyumba. Hili ni jambo linalohitaji mjadala zaidi. Bunju anajitokeza  kama mwanamume anayefanya majukumu yote ya kifamilia, hali ambayo  haimtayarishi mkewe kwa maisha ya baadaye iwapo mambo Kuna pia suala la  matumizi ya pesa ili kutibu magonjwa. Familia nyingi yataharibika. hazina bima  ya matibabu. Magonjwa yanapobisha hodi basi huziacha baadhi ya familia hizo  katika hali ya umaskini. Wengi huitisha michango kama Neema anavyoitisha  msaada kutoka kwa Bunju.  

🙓 Katika mazungumzo yao, pia inadhihirika wazi kwamba mapato ya kazi moja  hayatoshi kamwe. Umuhimu wa kujishughulisha zaidi ili kuweza kuyamudu  mahitaji unajitokeza.  

Onyesho II 

🕕 Sara yuko hospitalini ambako amelazwa. Neema na Asna wamefika kumwona.  Sara anataka kuruhusiwa kwenda nyumbani kwa sababu gharama ya hospitali  inaendelea kupanda. Sara analinganisha huduma za matibabu za kule kijijini na  za mjini. Hospitali za mjini ni kama hoteli ilhali za kijijini ni kama seli ambako  mtu akilazwa hata matumaini ya kupona hudidimia.  

🕕 Sara anataka atoke hospitalini arudi kijijini kwenda kumsaidia Yona ambaye  alimwachia kazi zote za nyumbani. Bunju anafanya shughuli zake bila kupita  hospitalini kumjulia hali Sara. Jambo hili linamkera Asna ambaye anamwona  Bunju kama mchoyo na asiyewajibika kuhusu mkwe wake. Neema anamtetea  

Bunju.  

 

🕕 Anasema kwamba tabia yake inatokana na jinsi alivyolelewa, kwa hivyo  wasimlaumu.  

Masuala makuu  

🙓 Mazungumzo haya yanaibua mambo matatu muhimu kuhusu hospitali  aliyopélekwa Sara. Mosi, malazi na chakula ni vya hali ya juu. Pili, gharama ya  huduma ni ya juu mno. Tatu, hospitali hiyo ina aina nyingi za wataalamu. Hali hii inakinzana na hali ilivyo katika baadhi ya hospitali nchini ambazo ni duni na  hutoa huduma mbovu zinazomfanya mgonjwa kutamauka na kukata tamaa.  

🙓 Hospitali za kibinafsi hutoa mazingira mema zaidi ya kimatibabu na ni mwafaka  zaidi kwa wale wanaoweza kulipia gharama zake, Mazingira ya hospitali za  umma ni duni, nyingi zikiwa hazina huduma bora, hazina madaktari na hata  dawa za kutosha.  

🙓 Pia, mwanamume angali anapewa hadhi ya juu kuliko mwanamke. Jamii  haimruhusu mwanamume kufanya kazi za jikoni kwa sababu kazi hizo  huchukuliwa kuwa ni za kike. Ndiposa, ingawa Sara angali mgonjwa, bado ana  ari ya kurudi nyumbani kumshughulikia Yona, mumewe.  

🙓 Bunju amechorwa kama mtu asiyemjali mama mkwe. Ingawa Neema  haridhishwi na hali hiyo, anashindwa kumkabili na kusingizia malezi.  🙓 Heshima anayopewa mwanamume na mwanamke katika onyesho hili,  inawekwa kwenye mizani.  

Onyesho III 

🙓 Neema anamsaidia Lemi katika masomo yake. Lemi analalamika kwamba kwa  muda mrefu wazazi wake hawajampeleka ziara. Neema anamweleza kuwa  hataweza kumpeleka ziara kwa sababu anamrudisha bibi kijijini. Lemi haelewi  ni kwa nini bibi yake hakuja kumsalimia.  

🙓 Neema anamwomba Bunju ampeleke Lemi kwenda kuogelea kwa kuwa yeye  anapanga kumrejesha mama yake nyumbani. Bunju anakataa kwa sababu ya  gharama na pia anasema anaenda kutafuta riziki. Analalamika kuwa Neema  mara nyingi yuko nje kikazi na anamwachia majukumu yote ya nyumbani.  

🙓 Bunju analalamika kwamba hakujulishwa kuwa mama mkwe ametoka  hospitalini na kwamba atasafirishwa kijijini. Neema anamwambia Bunju kuwa  mkewe hakutaka kumsumbua na mambo ya kwao nyumbani.  

🙓 Kulingana na Bunju, Neema ameanza kumdharau. Bunju anamkumbusha Neema  alivyokuwa mahututi wakati alipompata. Suala hili linamhuzunisha Neema hata  anaanza kulia. Bunju anamhurumia na kumwambia atulie asilie mbele yake.  

Tathmini  

Katika onyesho hili, suala la mivutano baina ya wanandoa kuhusu majukumu ya familia  yao linajitokeza. Ni bayana kwamba suala hili linahitaji tahadhari ili lisiwe chanzo cha  mafarakano katika ndoa. Pia, kuna suala la gharama za kulea watoto. Ni lazima wazazi  wawape muda wana wao kama Neema anavyomsaidia Lemi na kazi za shule. Lakini pia  kuna gharama nyingine za kuwafurahisha watoto ambazo zinahitaji pesa na mara  nyingi pesa hizo hazipo. Kwa hivyo, ni lazima kuwe na maelewano baina ya wazazi na  watoto kuhusu mambo hayo ili kusiwe na mikurumbano. Ni vyema pia wazazi  kuwaeleza watoto kuhusu gharama hizo ili wazielewe mapema. Onyesho hili linatukia  nyumbani kwa Asna. Sara na Asna  

Onyesho IV  

✹ wanazungumza. Mazungumzo ya mama na bintiye yanagusia masuala mengi.  Inabainika kuwa Asna hana imani na ndoa. Anaridhika na maisha ya kuishi bila  mume ingawa amefikia umri wa kuolewa. Kulingana na Asna, ndoa ya Neema ina doa. Hii ni kwa sababu Bunju ni bahili na hapendi wazazi wa Neema walale  nyumbani kwake. Pili, anaonelea kuwa, Sara pia aliteseka sana katika ndoa yake.  Hata ugonjwa alionao ulitokana na kero za Yona, baba yao. Asna anaamua kuishi  nje ya ndoa kwa sababu ya mifano ya ndoa hizo mbili zisizoridhisha. Katika  onyesho hili, Sara anapata muda wa kumzungumzia Asna masaibu ya ndoa yake  na babake na jinsi yalivyoanza.  

✹ Sara na Asna wanazungumzia juhudi za Dina na wanawe ambazo zimewasaidia  kujitoa katika lindi la umaskini.  

Masuala makuu  

🙓 Kulingana na Asna, taasisi ya ndoa ina uwezo mkubwa wa kumletea binadamu shida nyingi. Anamweleza mama yake kwamba msongo wa moyo alionao unatokana na  matatizo yaliyo katika ndoa yake. Pia, anaona kuwa ndoa ya Neema ina matatizo.  

Kwamba Bunju ni mchoyo na hajali ugonjwa wa mama yao, hali inayomfanya  Neema kutokuwa na raha katika ndoa yao. Mifano hiyo miwili inamfanya Asna  kutoridhishwa na asasi ya ndoa na hivyo, kuikinai. Lakini Sara anamweleza kuwa  ingawa ndoa huwa na changamoto nyingi, uvumulivu huwasaidia wanandoa  kukabiliana na changamoto hizo.  

🙓 Kulingana na Sara, bidii ni silaha inayoweza kumkomboa mwanadamu kutoka  umaskini. Familia ya Dina inatumika kama mfano wa familia ambayo awali ilikuwa  maskini lakini ikafaulu kujinyanyua kutoka hali hiyo ya umaskini na kujikimu  ipasavyo.  

🙓 Sara anamweleza Asna kuwa hata yeye (Sara) na mumewe Yona walikuwa maskini  lakini hawakusita kufanya bidii. Waliungana katika juhudi zao ili kujimudu katika  kuwatunza na kuwasomesha watoto wao hasa wakati Yona alipopoteza kazi yake ya ualimu. Hatimaye, watoto wao waliweza kuhitimu hadi Chuo kikuu. Inamsikitisha  kuwa wanajamii bado waliwachukulia kuwa maskini wa kutojaliwa kupata mtoto  wa kiume hata baada ya kufanya juhudi hizo zote. Suala la unyanyapaa dhidi ya  

 

familia za walevi linajitokeza pale ambapo familia ya akina Asna inadharauliwa na  kunyimwa hadhi katika jamii kwa sababu ya ulevi wa Yona.  

Sehemu IV  

Onyesho I  

🙓 Kijijini nyumbani kwa Luka. Luka anawakaribisha Beni na Yona kwa sherehe ya  kufurahia mazao yake. Beni anazungumzia jinsi watu walivyozitupa mila zao  kabisa. Anasema kwamba vizazi vijavyo havitakuwa na mila na desturi. Katika  mazungumzo yao, wazee hao watatu wanakubaliana kuwa vizazi vya siku hizi  vinafikiria kuwa uzungu ndio ustaarabu. Jambo hilo linatokana na malezi ya  mjini ambayo mara nyingi yameachiwa wafanyakazi wa nyumbani. Wazazi  wanaraukia vibaruani asubuhi na kurudi usiku watoto wakiwa wameshalala.  

🙓 Luka anawakumbusha wenzake kuwa mila za zamani hazikuwaruhusu watoto  wa kike kwenda shuleni wala kurithi mali ila walitegemea usaidizi wa waume  zao. Lakini anakubali kuwa thamani ya mtoto wa kike imepanda na nafasi yake  kupanuka. Watoto wa kike wa Yona wanamulikwa katika mazungumzo haya.  Japo walidharauliwa hapo awali, sasa wamekuwa nyota ya jaha. Ni wazi kwamba wao sasa ndio wanaogharamia matibabu ya mama yao katika hospitali za hali ya  juu huko mjini.  

🙓 Hata hivyo, fikra za kitamaduni bado zinatawala. Beni anamlaumu Sara kwa  kumwacha Yona peke yake akifanya kazi zote za nyumbani. Luka anapinga kauli  ya Beni ya kuwadunisha watoto wa kike na mwanamke kwa jumla.  

🙓 Katika onyesho hili, masuala ya ulevi na athari zake, taasubi ya kiume, usawa wa  kijinsia na mabadiliko yanaangaziwa.  

Masuala makuu  

Suala la utamaduni linajitokeza wakati wazee wanapotoa rai kwamba dini za  kisasa zimewafanya watu kudharau utamaduni wao.  

Yona na Beni wanalalamikia kukengeushwa kwa wanajamii. Wanaeleza kuwa  watoto wa siku hizi hawazifahamu lugha zao za kiasili, kwamba wamezama  katika Kiswahili na Kiingereza. Wanashindwa kutofautisha hata wanyama wa  kufuga kama vile mbwa, mbuzi na kondoo. Suala la usawa wa kijinsia  linazungumziwa kupitia maelezo kuwa wanawake wa zamani waliwategemea  waume zao lakini sasa jinsia zote zinachuma na kushirikiana katika malezi ya  watoto. Neema, anakuwa mfano mwema wa mwanamke aliyefaulu maishani na  ambaye anachuma na kuwatunza wazazi wake kama vile mtoto wa kiume  angalivyoweza kufanya. Nafasi ya mtoto wa kike katika maendeleo ya familia  inajitokeza. Ni wazi kwamba tofauti na zama za kale, watoto wa kike wa sasa  wamesoma na kuajiriwa, na kuwa tegemeo muhimu katika familia zao na jamii  nzima kwa jumla.  

Aidha, suala la chanzo cha ulevi wa kupindukia linamulikwa. Ni wazi kuwa  vijana wengi huingizwa kwenye mitego ya ulevi wanapotangamana na wenzao 

chuoni. Kwa wengine, mbegu hiyo ya ulevi huota na kuwa chanzo cha vurugu na  maangamizi maishani. Kutangamana kwa vijana katika taasisi za elimu kumeleta athari nzuri na mbaya kutegemea jinsi wanavyotumia uhuru wao.  

Onyesho Il  

🙓 Onyesho hili linatokea nyumbani kwa Sara, kijijini. Sara na Neema wanajadiliana kuhusu suala la utamaduni na mabadiliko ya kijamii.  

🙓 Neema anasema ulimwengu unakwenda mbio ilhali watu wengine wamebaki  nyuma katika mielekeo ya kijadi ya kubugia pombe bila kikomo.  

🙓 Sara anamtetea Yona kwa kutowajibika ipasavyo na majukumu ya nyumbani  hasa yale ya mifugo. Kulingana na Sara, mwanamume hawezi kuwekwa katika  kiwango kimoja na mwanamke. Anasema  

🙓 Yona anatekeleza majukumu yake ipasavyo. Hizo ni fikra za kitamaduni. Kwa  Sara, mwanamume ana nafasi yake katika jamii na hapaswi kumsaidia  mwanamke kazi za nyumbani. Kufanya hivyo ni kualika minong'ono ya  wanajamii na kuwakosesha wanawe waume wa kuwaoa.  

🙓 Sara anatunza heshima ya ndoa yake ili watoto wake wapate fanaka maishani  licha ya mateso anayopata kutoka kwa mumewe. Sara anampa Neema ushauri  unaoweza kuifanikisha ndoa yake. Anamshauri Neema azungumze na baba yake  kwa hekima ili amsaidie kubadilisha msimamo wake, hasa kuhusiana na ulevi.  

Masuala makuu  

🙓 Kwa mara nyingine, taasisi ya ndoa inazungumziwa. Ingawa wanandoa  wanapaswa kusaidiana, ni wazi kuwa jamii za Kiafrika bado zinatilia mkazo  mgawo wa kazi katika jamii. Kuna majukumu mengine ambayo jamii haitarajii  yafanywe na mwanamume mwenye mke, na iwapo ataamua kuyachangamkia,  basi inakuwa ni kama yanampunguzia hadhi katika jamii. Ingawa fikra hizo  zimepitwa na wakati na jamii imebadilika, bado jamii inatumia vigezo vya  tamaduni hizo kumwekea mipaka mwanamke. Hata hivyo, Sara anamuasa  Neema kuzitilia maanani tamaduni hizo ili kudumisha ndoa yake.  

🙓 Onyesho hili pia linazua suala la ukoloni mamboleo. Kutokana na mazungumzo  ya Sara na Neema, ni wazi kwamba matatizo ya kiuchumi ya mataifa machanga  yanasabishwa na hali ya mataifa hayo kuendelea kuwa masoko ya bidhaa za nchi za nje. Yamebakia tu kuwa masoko ya bidhaa zitokazo ng'ambo badala ya  kujibidiisha kuzalisha bidhaa zao.  

Onyesho III 

✔ Onyesho linafanyika asubuhi pale kijijini. Yona yuko peke yake sebuleni.  Ugonjwa wa mkewe unamhuzunisha na anajutia maisha yake ya awali  yaliyomletea mkewe ndwele. Neema anampata babake akiwa katika hali ya  mawazo mengi. Yona anashangaa kumwona bintiye amekonda.  

 

✔ Yona anamwelezea Neema jinsi maradhi ya Sara yalivyoathiri mji wake.  Anamshukuru kwa kumshughulikia mamake.Yona anakumbuka maisha yake ya  chuoni na jinsi alivyokuwa mwerevu. Neema anapata mshangao anapogundua  kuwa babake ameandaa kiamshakinywa mapema, yeye na mama yake wakiwa  bado wamelala. Neema anafurahi na kumshukuru babake kwa wema wake.  

✔ Onyesho linaisha kwa kuonyeshwa Yona akiomba msamaha kwa Neema kwa  makosa aliyowafanyia wakiwa wangali wachanga. Yona anatumai kuwa mabinti  wake wengine watamsamehe siku moja. Yona pia anaomba msamaha kwa mke  wake na kumwahidi kuwa asitie shaka atakuwa naye katika kila hali. Taa  zinazima na wote watatu wanakumbatiana kuonyesha hali ya kusameheana na  kuja pamoja kwa familia hiyo.  

Masuala makuu  

Katika onyesho hili, Yona anapata fursa ya kujirudia na kufikiria maisha yake ya siku za  usoni. Anatambua kuwa mke wake ni mgonjwa kwani sasa maisha yake yanaendeshwa  na madawa. Anaamua kuacha kunywa pombe kabisa. Uamuzi wa Yona una umuhimu  mkubwa kwa sababu anakubali kuwa alimkosea mkewe na kwamba umefika wakati wa kujutia makosa hayo na kuanza upya. Kupitia kwa Sara na Neema, anaonekana kuomba  msamaha familia yake kwa yote aliyowatendea na kuwaomba wampe nafasi ya kuanza  maisha yake upya. Hii ni hatua kubwa na mwafaka katika maisha ya Yona na familia  yake. Anaahidi kumtunza mkewe kikamilifu.  

MSUKO  

Kazi ya fasihi huwa imepangwa kwa muundo maalumu. Muundo huu huitwa msuko.  Msuko ni mtiririko wa matukio katika kazi ya fasihi, Ni namna kazi ya fasihi huwa  imepangwa kutoka mwanzo hadi mwisho.  

Msuko huwa na sehemu tatu kuu ambazo ni:  

a) utangulizi/ mwanzo/ ufunguo  

b) kati/ sehemu ya pili- kilele na mpomoko  

c) hitimisho/ mwisho  

a) Utangulizi/mwanzo  

o Mwanzo katika tamthilia hii unaanza kwa kueleza uhusiano uliopo bainaya  wahusika. Hivyo basi, utangulizi huu unatusaidia kujua uhusiano wa wahusika.  Kwa mfano, mwandishi wa tamthilia ya Bembeaya Maisha ameonyesha  uhusiano wa wahusika kama vile: Sara na Yona ambao ni mke na mume na  waliobarikiwa na watoto watatu wa kike ambao ni  

o Neema, Asna na Salome. Mhusika Dina ameelezwa kama mama yake Kiwa na  rafikiye Sara. Bunju ni mumewe Neema; wamejaliwa na watoto wawili ambao ni  Mina na Lemi. Beni na Luka wanatajwa kama wazee wa kijiji.  

 

o Utangulizi au mwanzo wa tamthilia ya Bembea ya Maisha unamsaidia msomaji  kujua uhusiano uliopo bainaya wahusika najinsi wanavyoshiriki katika kitabu.  o Sehemu ya utangulizi pia humsaidia msomaji kujua mahali na wakati mchezo  unafanyika. Tamthilia ya Bembea ya Maisha ni mchezo/kazi ya fasihi  inayofanyika katika eneo la Afrika wakati wa jana na leo.  

o Utangulizi katika tamthilia hii pia unamwezesha msomaji kupata kiini cha  mchezo. Kiini katika tamthilia ya Bembea ya Maisha kinajitokeza katika onyesho  la kwanza na la pili. Kulingana na tamthilia hii, kiini chake ni pamoja na namna  utamaduni, mila na desturi za jamii husika zinavyoweza kuidunisha familia.  

b) Kati/sehemu ya pili  

🙓 Sehemu hii huwa imegawika katika sehemu mbili ambazo ni kilele/ upeo na  mpomoko. Msomaji hupata mivutano au migogoro baina ya wahusika. Sehemu  hii inasaidia kuibua maudhui katika kazi ya fasihi.  

🙓 Katika tamthilia ya Bembea ya Maisha, sehemu ya kati inajidhihirisha katoka  sehemu ya Il kuendelea.  

🙓 Mivutano baina ya wahusika inajidhihirisha kupitia wahusika kama vile Sara na  Asna kuhusu suala la ndoa. Wawili hawa wana mitazamo tofauti kuhusiana na  suala la ndoa. Asna ana mtazamo hasi ilhali Sara ana mtazamo chanya. Sara  anamtaka Asna aolewe ili amletee mjukuu ampakate kwa mikono yake kabla  hajaaga dunia. Hata hivyo, Asna anaona ndoa kama suala la kuleta matata katika  familia. Mtazamo huu unachochewa na jinsi ndoa ya wazazi wake na ile ya  dadake zinavyojidhihirisha. Asna anaona kuwa ndoa imemuweka mama yake  katika hali ya ugonjwa atakaoishi nao milele (uk. 54). Vilevile, kulingana na  Asna, ndoa imemfanya Neema kutokwa na hali ya ukakamavu na kujiamini kwa  dhati (uk. 54).  

🙓 Maudhui yanayojitokeza katika sehemu hii ni ndoa, utamaduni, taasubi ya  kiume, nafasi ya mwanamke na mengineyo.  

Kilele/ Upeo  

✔ Kilele katika tamthilia ni sehemu ambayo matukio yanafanyika katika hali ya  taharuki. Msomaji akifika katika sehemu hii, hupatwa na mshawasha wa kutaka  kusoma ili apate ujumbe kamili.  

✔ Katika tamthilia hii ya Bembeaya Maisha, sehemu ya kilele inajitokeza katika  mazungumzo ya Dina na Sara. Ni baada ya mazungumzo hayo, ndipo msomaji  atapata hamu ya: kutaka kujua namna walivyofanikiwa, kujua kama ugonjwa wa  Sara utapona, kujua kama ulevi wa Yona ulipungua au ulifikia kikomo. Msomaji  anapata hamu ya kujua kama mtazamo wa jamii kuhusu familia ya Yona na Sara  ulibadilika au uko vilevile.  

Mpomoko  

Hii ni sehemu ambayo mhusika mkinzani anashindwa. Katika sehemu hii,  tensoni/msuko wa tamthilia unashuka.  

Mpomoko katika tamthilia hii ya Bembea ya Maisha unajidhihirisha wakati Yona  anapokuwa akijizungumzia na kujilaumu kwa kukosa kumshughulikia mkewe Sara  (uk. 70). Yona anakata shauri ya kutoshiriki katika unywaji wa pombe. Anasema  kuwa atatumia siku zake kumwangalia mke wake mgonjwa. Hapa ndipo msuko wa  tamthilia unashuka kwa kuwa msomaji ameshapata suluhu ya tensoni au taharuki  aliyotaka kujua itaishia wapi.  

c) Mwisho/Hitimisho  

Hii ni sehemu ya mwisho katika msuko wa tamthilia. Sehemu hii inamwezesha msomaji kujenga au kupata suluhu ya suala kuu linalojitokeza katika tamthilia. Mwisho wa  mchezo wa Bembea ya Maisha unajitokeza Yona anapoomba msamaha kwa mwanawe  Neema na kutumainia kuwa wanawe wengine watakuja kumwelewa. Aidha, anaomba  msamaha kwa mkewe kwa kutomjali siku za awali. Anamwahidi kuwa atasimama naye  katika kila hali (uk. 74).  

MAUDHUI NA DHAMIRA  

Maudhui ni masuala muhimu ambayo mwandishi anayachanganua Maudhui katika kazi yake; yale mambo muhimu anayoyaona katika jamii na anayotaka kuyaeleza kisanaa  katika kazi yake, bila kujali utanzu anaotumia kumulikia masuala hayo. na namna  mwandishi anavyoyajadili. Msomaji anaweza kuelewa lengo la mwandishi na funzo la  kazi yake kupitia jinsi anavyochanganua masuala  

Katika tamthilia hii, mwandishi ameshughulikia masuala yafuatayo: mbalimbali.  mabadiliko, migogoro, ndoa na mahusiano katika ndoa, nafasi ya mwanamke katika  jamii, tamaduni, maadili ya kazi, ulevi, maendeleo, malezi na bidii maishani.  

1. Nafasi ya mwanamke  

Haya ni maudhui yanayonyesha namna mwanamke amesawiriwa katika tamthilia ya  Bembea ya Maisha.  

🙓 Mwanamke amesawiriwa kama mwerevu na mwenye maarifa, hekima na  busara. Kwa mfano, katika uk. 6 Kiwa anasema kuwa Sara amebarikiwa na  watoto wenye akili nzuri. Wote wamehitimu vizuri na kuleta faraja. Tunaona  Neema amesoma na kuhitimu Chuo kikuu na ana kazi nzuri. Asna na Salome  vilevile wamefanikiwa kusoma hadi Chuo kikuu. Salome alipita mtihani kwa  kupatafirst class. Alibahatika kwenda nwambo kuendeleza masomo yake (uk.  28).  

🙓 Mazungunzo ya Sara katika tamthilia hii yanaonekana kuwa yenye wingi wa  hekima na busara. Anatoa ushauri katika masuala mbalimbali kama vile:  masuala ya ndoa, maisha, heshima na mengineyo.  

 

🙓 Mwanamke anaonekana kama mzazi anayestahili kujifungua watoto wa kike na  wakiume na hasa watoto wa kiume. Asipopata watoto wa kiume, anasutwa na  kukejeliwa.  

🙓 Tunaelezwa kwamba Sara alisutwa na kutukanwa na wanajamii kwa kukosa  mtoto wa kiume hata baada ya kujaliwa na mabinti watatu baada ya muda mrefu bila watoto (uk. 6,7).  

🙓 Mwanamke amesawiriwa kama mtu mvumilivu na anayestahili kuvumilia  mateso na bughudha za ndoa. Kwa mfano, Sara anavumilia ndoa yake ambayo  ilikuwa na changamoto nyingi. Aidha anavumilia mumewe Yona baada ya  kumtesa na kumchapa kichapo cha mbwa.  

🙓 Neema anapewa mawaidha na mama yake kuhusu kuzidi kuvumilia ndoa yake.  Kudhihirisha suala hili la uvumilivu wa ndoa tunamwona  

🙓 Neema akimweleza mumewe kwamba anakubaliana na wazo kuwa hawaishi  katika ndoa ya raha mustarehe mia fil mia (uk. 48). Wazo hili linaonyesha kuwa  Neema pia anavumilia ndoa yake na Bunju.  

🙓 Mwanamke ameonyeshwa kama mtu anayestahili kujukumika katika majukumu  ya nyumbani. Anasawiriwa kama mtu mwenye majukumu ya shambani, jikoni  na nyumbani kwa jumla. Yona anapomkuta Sara ameketi, analalamika kuwa  hajaandaliwa chochote. Inambidi Sara amtumie salamu Dina ili aje amsaidie  kupika. Hali hii inaonyesha kuwa ni jukumu la mwanamke kupika na kuandaa  chakula kwa mumewe.  

🙓 Kizazi cha jana kimemsawiri mwanamke kama mtu asiyestahili kupata elimu.  Sara anasema kuwa siku zao elimu ya wasichana ilifanywa bezo. Yeye aliachia  darasa la saba (uk. 33).  

🙓 Mwanamke amesawiriwa kama kiumbe dhaifu. Kiumbe ambacho hakifai  kushindana na mwanamume. Sara anamwambia bintiye  

🙓 Neema kuwa utamaduni ungali una nguvu na hawezi kushindana na  mwanamume (uk. 66).  

🙓 Wanawake katika tamthilia hii wameonyeshwa kama watu wenye msimamo  dhabiti. Sara na binti zake wamesawiriwa kama wenye msimamo imara. Kwa  mfano, Sara anasimama na familia yake hata baada ya kutukanwa na kukejeliwa  na wanajamii. Hakuwacha familia yake, alisimama nayo hadi wakati wa mwisho.  Asna pia ana msimamo wake kuhusu ndoa (uk. 53). Anashikilia msimamo kuwa  ndoa ni taasisi inayomkandamiza mwanamke na kuwa haifai.  

Mabadiliko  

Mabadiliko ni hali ya kutoka katika hali moja hadi nyingine. 

a) Mabadiliko yanajitokeza pale ambapo Yona anatueleza kuhusu maisha yake ya  ujana alipokuwa mwalimu. Anatueleza namna alivyokuwa akiamka alfajiri na  mapema kiboko mkononi na mwanafunzi aliyekuja baada yake angepokea  kichapo. Anasema kuwa siku hizi huwezi kumnyoosha mtoto kwa kiboko. Suala  hili linamaanisha kuwa kuna mabadiliko ya sheria na kanuni za shuleni (uk. 62).  

 

b) Suala la mabadiliko linadhihirika wakati Yona anakubaliana na Sara. Mtazamo wa  Yona kwa Sara unabadilika. Alikuwa hana huruma kwa mkewe Sara alipokuwa  mgonjwa. Katika onyesho la kwanza, Yona analalamika kwa sababu Sara alikuwa  hajamwandalia chakula. Yona alikuwa hana huruma hata baada ya Sara  kumwelezea kuwa alikuwa hajaandaa chakula kwa sababu ya maumivu (uk. 1).  

c) Mabadiliko yanajitokeza wakati Yona anaonekana kuhuzunishwa na maradhi ya  mke wake. Anasema aliona hapo awali kama maradhi yale yalikuwa mchezo lakini  sasa anatamani angeishi tofauti. Yona anasema hawezi kuendelea kuishi kama  zamani, ni lazima angefuata mkondo mpya wa maisha. Anataka kuzitumia siku  zake za uzee kumshughulikia mkewe (uk. 70). Anamwambia Sara pole na kusema  kuwa taabu zake Sara zitakuwa taabu zake (uk. 74).  

d) Yona amesawiriwa kukuza maudhui ya mabadiliko. Mwanzoni, ameonyeshwa  kama mtu mzuri, baada ya kusutwa na kudharauliwa kwa kukosa mtoto wa kiume  anabadilika na kuwa mlevi na kupoteza upendo kwa familia yake. Tunamwona  akimpokeza bibiye kichapo cha mbwa hadi kusababishia bibiye maradhi ya moyo.  Yona anabadilika kutoka hali hiyo ya ulevi kwa kuamua kuchukuwa mkondo mpya wa maisha (uk. 70). Anasema kwamba pombe imemchezesha kama mwanasesere  na kumnyima fursa ya kuilea familia yake.  

e) Kuna mabadiliko ya mitazamo ya utamaduni wa jamii ya kizazi cha jana na ya  kizazi cha leo. Mabadiliko haya yanajidhihirisha kupitia suala la mtoto wa kike na  mtoto wa kiume. Mtazamo wa mtoto wa kike katika kizazi cha jana umebadilishwa na utamaduni wa kizazi cha leo. Kizazi cha jana kinamwona mtoto wa kike kama  mtoto asiyekamilika na asiyestahili kusomeshwa wala kurithi mali ya familia (uk.  60). Wazo hili linabadilishwa na kizazi cha leo ambacho kinamwona mtoto wa kike sawa na mtoto wa kiume. Kwa hivyo, kama mtoto wa kiume, yeye pia anaweza  kurithi mali ya familia na vilevile kusomeshwa.  

f) Mabadiliko ya utamaduni pia yanajitokeza katika suala la ndoa. Sara anamweleza  Asna kuwa zamani, wasichana walikuwa wakiozwa punde tu walipobaleghe (uk.  52). Mtindo huu unabadilika miongoni mwa kizazi cha leo kwani wasichana  wanaolewa wakati watakapo.  

g) Mabadiliko ya utamaduni yanadhihirika kutoka kwa mhusika Yona ambaye, hapo  awali, hangeweza kuingia jikoni kumpikia mkewe Sara. Baada ya kugundua kuwa  hayo ni mambo yaliyopitwa na wakati, tunamwona akiandaa kiamshakinywa kwa  familia yake. Pia, anamhakikishia Sara kuwa atamshughulikia kwani hali yake Sio  nzuri (uk. 62).  

h) Kuna mabadiliko ya mitazamo au uonevu wa mambo katika tamthilia hii. Neema  anabadilisha mtazamo wake kuhusu baba yake (uk. 72). 

i) Bunju pia anabadilisha mtazamo wake wa kutomsaidia Neema kugharamia  matibabu ya mamake Sara. Anamwambia anaenda kukutana na mkurugenzi wa  kampuni na kuwa akipata hela, atampiga jeki katika suala la matibabu ya mama  yake (uk. 40).  

 

j) Tamthilia ya Bembeaya Maisha inaangazia mabadiliko ya maisha. Mabadiliko haya  yanajitokeza kupitia familia ya Yona. Kwanza, maisha ya Sara, mkewe Yona,  yanabadilika kutoka kuwa ya afya njema na kuwa yenye afya duni. Afya ya Sara  inazorota kutokana na ugonjwa wa moyo ambao ataishi akimeza vidonge vya  dawa maisha yake yote (uk. 71).  

k) Pia, mtazamo wa wanajamii kuhusu familia ya Yona unabadilika pia. Wanajamii  sasa wanaiheshimu familia ya Yona ambayo ilikuwa imedharauliwa na  kudunishwa hapo mbeleni. Familia hii haisutwi wala kutukanwa kwa sababu ya  mafanikio na elimu ya mabinti wao. Jambo hili linadhihirishwa kupitia maneno ya  Luka wakati walikuwa wakiongea na Beni na Yona.  

Ndoa  

Mwandishi amesawiri suala la ndoa kupitia wahusika wafuatao:  

🙓 Yona na Sara, Neema na Bunju na hata Asna. Kupitia ndoa za wahusika hawa  masuala mengi ya mahusiano katika ndoa yanajadiliwa.  

🙓 Ndoa ya Yona na Sara inasawiriwa kama ndoa ya kizazi cha jana.Inaonyesha  matarajio ya ndoa kulingana na jamii yao. Inaakisi malezi, majukumu ya mke na  mume na matarajio ya wanajamii kuhusiana na watoto. Inachora picha ya  majukumu kama yalivyopangwa na jamii ya Yona na Sara.  

🙓 Kulingana na jamii katika tamthilia ya Bembea ya Maisha, mwanamke  anapoolewa anahitajika kuanzisha familia na mumewe. Anatarajiwa kujifungua  watoto wa kike na vva kiume. Katika ndoa ya Yona na Sara, tunafahamishwa  kuwa wanajamii waliwasema na kuwatafuna kama chingamu huku Yona akiitwa gumba na Sara kuitwa tasa. Hii ni baada ya kuoana na kukaa kwa muda mrefu  bila kujaliwa na watoto (uk. 6). Ni wazi kwamba ndoa ya Yona na Sara  imenyimwa hadhi katika jamii kwa kukosa mtoto wa kiume (uk. 7).  

🙓 Kulingana na kizazi cha jana, mke anatarajiwa kujifungua watoto wa kike na wa  kiume na hasa wale wa kiume. Ndoa ya Yona na Sara inasutwa na kukejeliwa na  wanajamii kwa kukosa mtoto wa kiume ambaye aliaminika angekuwa mrithi wa  Yona (uk. 8). Wanajamii walimtaka Yona kumwoa mke ambaye angemzalia  watoto wa kiume. Kulingana nao, Sara alikuwa ameshindwa kumzalia mtoto wa  kiume. Unyanyapaa huu ulimsukuma Yona kuupokea ulevi na kuanza kumpiga  Sara kipigo cha mbwa kwa kuwa hakumzalia mtoto wa kiume (uk. 9-10).  

🙓 Ni wazi kwamba ndoa ya Yona na Sara imenyimwa nafasi na hadhi katika jamii  kwa kukosa mtoto wa kiume.  

🙓 Ndoa pia imesawiriwa kama kitu chema ingawa chenye changamoto zinazoweza kuvumiliwa. Sara anasema kuwa ndoa ni uvumilivu na wala Sio watoto na  hakuna ndoa isiyokosa doa. Sara anaivumilia ndoa yake na Yona. Anavumilia  kuchapwa, kudharauliwa na kudhulumiwa. Sara anamvumilia mumewe hata  baada ya dhiki hizo. Fauka ya hayo yote, anamshauri Neema aivumilie ndoa yake na Bunju. Vilevile, anamshauri Asna kumtafuta mume aolewe (uk. 33, 67).  

 

🙓 Ndoa huakisi suala la malezi. Yona na Sara wanaonyesha malezi kwa kuwalea  mabinti wao. Sara anawafurahia watoto wake na kujitahidi kuwalea ipasavyo.  🙓 Ndoa ya Neema na Bunju ni ya kizazi cha leo. Neema na Bunju wamesoma,  wamehitimu na wameajiriwa na kuanza familia yao. Wanashirikiana katika  masuala ya matumizi ya pesa. Bunju anashughulikia majukumu ya familia yake  na Neema. Amemruhusu  

🙓 Neema kutumia mshahara wake kuwasaidia wazazi wake. Ndoa katika tamthilia  hii imesawiriwa kama uhusiano unaofaa kuleta heshima na uvumilivu. Bunju  anamlalamikia Neema kwa kukosa kujulishwa kuwa mama mkwe wake anarejea kijijini bila yeye kujulishwa. Suala hili linamkera sana Bunju na kumuona Neema  kama mke asiye na heshima (uk. 48).  

🙓 Neema anasisitiza kuwa amempa mumewe heshima ya kutosha (uk. 49). Jambo  la ndoa limesawiri majukumu ya mke na mume. Katika ndoa  

🙓 ya Bunju na Neema, mume ana majukumu ya kulipa karo, kulipa kodi ya nyumba na majukumu mengine. Jambo hili linaonyesha kuwa Bunju ni mume  aliyewajibika. Kwa upande mwingine, Neema ana jukumu la kuwatunza wazazi  wake.  

🙓 Katika ndoa ya Sara na Yona, Yona anasawiriwa kuwa na jukumu la  kuwasomesha wanawe. Hata baada ya Sara kwenda mjini kwa ajili ya matibabu,  Yona anachukua majukumu nyumbani kama vile kushughulikia mifugo na  kuondoa mtama shambani. Katika mwisho wa tamthilia, Yona anamwahidi Sara  kuwa atayachukua majukumu yote kama mumewe na atamshughulikia katika  kila hali. Yona pia anaonyeshwa kuwa na jukumu la kumjuza Sara kuhusu  mikutano ya vyama vya kina mama.  

🙓 Ndoa pia imesawiriwa kama jambo lililojaa bughudha. Kulingana na Asna, ndoa  ina mateso na imejaa masharti mengi. Asna anaona ndoa ya dadake Neema  imejawa na matatizo yasiyoweza kuvumilika. Anasema kuwa Bunju ni mchoyo  na asiyetaka kumsaidia mtu (uk. 33, 45). Asna vilevile anaiona ndoa ya wazazi  wake kama iliyojawa na mateso.  

🙓 Anamweleza mamake kuwa amedhoofishwa na mateso aliyoyapata katika ndoa  yake (uk. 53). Hali hii inamfanya Asna kusawiriwa kama msichana anayetaka  kuyajenga maisha yake bila mume.  

Ulevi  

🙓 Maudhui ya ulevi yameangaziwa kupitia mhusika Yona. Tunaelezwa kuwa Yona  alijiingiza katika ulevi baada ya kushinikizwa na wanajamii kumuoa mke  mwingine atakayemzalia mtoto wa kiume. Shinikizo hili lilimfanya kuingilia  ulevi kwa hali ya juu zaidi.  

🙓 Kutokana na ulevi, alianza kumpa mkewe Sara kichapo cha mbwa (uk. 10).  Tatizo hilo la ulevi linamwingiza kwenye matatizo chungu nzima.  

🙓 Yona pia alifutwa kazi kwa sababu ya ulevi (uk. 56).  

🙓 Ulevi uliyamega maadili ya Yona na kumpokonya uwajibikaji wa familia yake.  Katika jamii yoyote ile, uraibu wa pombe uliopindukia unaweza kuwa chanzo  cha matatizo mengi katika familia. Yona anafutwa kazi na kuingia katika limbi la  uchochole.  

🙓 Anaanza kumdhulumu mke wake hadi kumsababishia maradhi ya moyo. Kwa  kifupi, pombe inayavuruga maisha yake kama mfanyakazi na kama mume  aliyetegemewa na jamaa yake.  

Teknolojia na Maendeleo  

✹ Suala la teknolojia na maendeleo limeonyeshwa na mwandishi kupitia maelezo  ya wahusika kama vile: Neema, Asna, Sara, Luka na wahusika wengineo.  ✹ Maendeleo ya mjini na kijijini yamedhihirishwa kupitia mazungumzo ya Neema  na Sara. Sara alikuwa amewasili mjini kwa ajili ya matibabu.  

✹ Neema anasema kuwa maendeleo mjini ni ya hali ya juu. Anasema kuwa watu  hufika mjini kutoka mashambani ili kupata jambo au kitu kizuri.  

✹ Anasema kwao maendeleo bado na yanakuja kwa kudoda (uk. 17). Hali  kadhalika, maendeleo ya kijijini yamedorora kwa sababu ya ahadi zisizotimizwa. Sara anasema kuwa tangu wakiwa watoto maendeleo yamekuwa yakija hadi  walipokuwa wazima na kujaliwa na watoto na ahadi hii ya maendeleo imebaki  kuwa tu ahadi isiyotimizika wakati wa uhai wao (uk. 17).  

✹ Katika mazungumzo ya Dina na Sara pale jikoni, Dina anasema kuwa anasikia  mjini kuna magari mengi, majengo makubwa, barabara nyingi na pia watu wengi (uk. 15). Mazungumzo hayo yanaonyesha namna mjini kulivyoendelea. Dina  anasema kuwa anasikia watu wa mjini wameendelea sana hata wametengeneza  magari yatembeayo hewani.  

✹ Maendeleo katika hospitali za mjini yamesawiriwa katika mazungumzo ya Sara.  Anasema kwamba kwenye hospitali aliyokuwa amelazwa, huduma za huko ni  nzuri sana mpaka anashindwa kuamini kama kweli yuko wodini. Anasema kuwa  kuna kitanda kizuri, godoro nzuri na shiti nzuri zilizoplgwa pasi. Anasema kuwa  madaktari hawakawii kuzibadilisha shiti hizo. Anasema hospitali za mjini si  kama za kijijini ambazo amezisawiri kama seli na ukilazwa katika hospitali hizo  tayari wewe ni kama mahabusu. Asna anasema kuwa hewa katika wodi za  hospitali za kijijini huwa zimejaa harufu ya dawa, vitanda vimesalimu amri  mpaka shiti zimekagura. Anasema kuwa hospitali hizo hazimpi mtu matumaini  ya kutoka akiwa bora na kumbidi mtu kuweka tumaini lake katika sala (uk. 42).  

Mawaidha au Wosia  

🕮 Suala la mawaidha au wosia katika tamthilia ya Bembea ya Maisha linakuzwa na  wahusika kama vile Luka, Yona, Sara na Neema. Sara anamwambia Neema kuwa  asishindane na mwanamume hasa nyumbani ila wanaweza shindana kazini au hata masomoni. Sara anawapa Neema na Asna mawaidha kuwa ni vyema  wamheshimu Bunju kama ndugu yao.  

🕮 Sara anawapa mawaidha wanawe wamheshimu baba yao aliyewalea na  kuwasomesha. Sara anawashauri Asna na Neema kuziheshimu na kuzitii mila na  desturi za jamii yao. Luka anawashauri Beni na Yona kuhusu I-muhimu wa elimu ya mtoto wa kike katika jamii. Anadai kuwa tamaduni, mila na desturi zinazidi  kubadilika na wanapoyapuuza hayo yote ni kazi bure (uk. 60). Luka awafundisha Beni na Yola kuhusu usawa kati ya watoto wa kike na wa kiume (uk. 60).  

🕮 Kuna mawaidha Sara anayompa Neema kwa njia ya mafumbo kuhusiana na  maisha. Sara anamweleza Neema kuwa hakuna kizuri kinachokuja kwa urahisi.  Analinganisha maisha na mbegu iliyopandwa. Mbegu hiyo hukua na kutoa mche  wenye umbo la kupendeza hata baada ya kuoza. Vivyo hivyo, maisha hukumbwa  na pandashuka lakini huzidi kuendelea. Anawataka Neema na dada zake warudi  kijijini kuotesha mbegu zingine zitakazokua na kuwa miche ya kupendeza kama  wao (uk. 68).  

🕮 Sara anampa bintiye Neema mawaidha ya jinsi ya kuelimisha wanakijiji na  kuwapa maarifa ya kisasa. Anamwambia anaweza kuanza kwa kumshawishi  baba yao badala ya kumkabili kumwelewa ndiposa aweze(uk. 69). 

Malezi  

🕕 Suala la malezi limejitokeza kupitia kwa wahusika Yona na Sara, Bunju na  Neema na hata Bela. Yona na Sara wanajikakamua kuwalea watoto wao kwa njia  inayostahili. Wawili hao walikuwa hawajiwezi kiuchumi hasa baada ya Yona  kufutwa kazi kutokana na ulevi. Wanajitahidi kuwasomesha watoto wao.  Kifungua mimba wao, Neema, alisoma hadi Chuo kikuu na kupata shahada mbili. Wanawalea mabinti hao badala ya kuwaelekezea ndoa za mapema kama njia  moja ya kutoroka uhitaji wa kiuchumi waliokuwa nao.  

🕕 Neema na Bunju wanaonyesha malezi kwa kuwasomesha ndugu za Neema hadi  kuhitimu Chuo kikuu. Bunju anasema kuwa waliishi na Salome huku wakimlipia  karo ya shule ya upili na chuoni (uk. 28). Bunju na Neema vilevile wanamlea  mtoto wao Lemi. Wanamsaidia kufanya kazi ya ziada ya shule.  

🕕 Bunju na Neema wanasawiriwa kama wazazi ambao hawajawajibika katika  kuwalea watoto wao kikamilifu. Wanamwajiri Bela ili awasaidie katika ulezi wa  Lemi na shughuli za pale nyumbani. Mtoto wao Mina anasoma katika shule ya  bweni, kwa hivyo mara nyingi hayuko nyumbani bali yuko shuleni. Hii ina  maana kuwa malezi ya Mina yanatekelezwa na walimu wake. Vilevile, Neema  anahuzunishwa na jinsi anavyokosa muda wa kuonana na mwanawe Lemi. Mara nyingi akitoka asubuhi Lemi huwa amelala na akirudi vilevile huwa amelala (uk.  22).  

🕕 Bunju anasema kuwa mara nyingi Neema hayupo nyumbani na kuwa yeye ndiye  humsaidia Lemi kufanya kazi ya ziada (uk. 49).  

🕕 Bela anakuza maudhui ya malezi kwa sababu ameajiriwa kama mfanyakazi  nyumbani kwa Neema. Bela ameiacha familia yake na kuja kuifanya kazi ya  kumlea Lemi. Bela amezoeana sana na Lemi kuliko alivyozoeana na mamake  Neema. Bela anamfahamisha Neema jinsi Lemi anavyoendelea. Anamwambia  kuwa Lemi alikuwa amekula na keshalala kwa sababu ya uchovu uliotokana na  mazoezi ya shuleni. Bela anasema kuwa kila baada ya kutoka shule, Lemi  humwonyesha jinsi walivyocheza shuleni. Hii ina maana ya kuwa Bela ndiye  aliyekuwa mlezi wa karibu wa Lemi.  

🕕 Yona anamsifia Sara kwa kumsaidia katika kuwalea na kuwasomesha mabinti  wao. Anasema alikuwa akiwaangalia ng'ombe shambani huku Sara akipeleka  maziwa na kuuza bidhaa walizozalisha sokoni (uk. 62).  

🕕 Malezi katika maisha ya mjini yanasawiriwa kama ya ajabu. Yona anasema kuwa malezi mjini ni magumu sana. Watu wa mjini huraukia vibarua na kurudi watoto wakiwa wamelala. Wanaishi wiki nzima hawajaonana na watoto wao. Malezi  yameachiwa yaya. Yaya ambaye anaweza kumfundisha mtoto lugha au tabia  aitakayo. Ulezi umejaa mashaka (uk. 59).  

Taasubi ya Kiume  

o Taasubi ni hali ya jamii kuthamini jinsia moja kuliko nyingine. Jamii katika tamthilia  ya Bembeaya Maisha imemthamini mwanamume kuliko mwanamke kwa njia  zifuatazo.  

o Mwanamume amesawiriwa kama mtu anayeweza kurithi mali ya familia. Hii ni  kuonyesha kuwa mwanamume tu ndiye mwenye uwezo huo (uk. 2). o Sara anasema fimbo hurithiwa na watoto wa kiume wala si wa kike. Jamii  inamshinikiza Yona kuoa mke mwingine ili aweze kumzalia mtoto wa kiume  ambaye atakuwa mrithi wa fimbo yake.  

o Mwanamume ameonyeshwa kama mtu asiyestahili kuhusika na kazi ambazo  zinaaminika ni za mwanamke. Kazi kama vile kupika na kuteka maji kisimani ni kazi ambazo zinaamika kuwa kazi za wanawake.  

o Beni anamwambia Yona amekaa muda mwingi kama mkewe hayuko nyumbani.  Beni anamuuliza Yona nani anayempikia muda wote huo kwani umri wake si wa  kuingia jikoni kujipikia (uk. 61).  

o Sara naye anamkaripia mwanawe Asna ambaye anasema haoni ubaya wa baba yake  kwenda kujitekea maji kisimani. Sara anasema kwamba itakuwa aibu kubwa na  wanajamii watamtazama Yona kwa dharau (uk. 44-45).  

o Katika uk. 1, tunamwona Yona aliyekinai na kukasirishwa na Sara ambaye ameketi  palepale ilhali hajamwandalia chakula. Yona hajali kuwa mkewe anaugua, haja yake  ni chakula. Kwa sababu ya mila za jamii, Yona hawezi kuingia jikoni kuandaa  chakula. Inamlazimu Sara kumwita Dina ili aje amsaidie katika maandalizi ya  chakula. Suala hili limetiliwa mkazo katika mazungumzo ya Sara na Dina (uk. 14),  kuwa mwanamume hawezi kusaidia katika kazi zozote za jikoni.  

 

Utamaduni  

o Utamaduni una nafasi muhimu katika jamii ya Sara na Yona. Wanajamii wanaamini  kuwa kuna mafunzo mengi ambayo yanatokana na mila na desturi za jamii hiyo.  o Katika jamii ya Yona na Sara, kuna msisitizo mkubwa kwamba kila familia sharti iwe 

na mtoto wa kiume. Familia zenye watoto wa kike peke yake zinadhihakiwa na  kudharauliwa kama ilivyofanyiwa familia ya Yona na Sara. Luka anapinga mwelekeo huu na kuwathamini watoto wa jinsia ya kike (uk. 60).  

o Utamaduni unajitokeza katika baraza la wazee: Luka, Beni na Yona. Luka  anawaalika wazee wenzake ili kunywa, kucheza na kufurahia mazao yao (uk. 64).  o Luka anataja kuwa mavuno ya kwanza huonjwa na wazee na kutoa baraka (uk. 58).  o Utamaduni unasawiriwa kama jambo lililopitwa na wakati kulingana na ulimwengu  wa leo. Kwa upande mwingine, utamaduni unazidi kutiliwa mkazo katika  ulimwengu wa jana. Bunju anakubaliana na utamaduni wa kutowakubali wazazi na  wakwe zake kulala nyumbani kwake.  

o Bela na Neema kwa upande mwingine wanapinga mawazo hayo na kusema kuwa  utamaduni huo umepitwa na wakati na kuwa hauna nafasi katika ulimwengu wa leo uliojaa mabadiliko ya kila aina (uk. 24, 29).  

o Asna anasema kuwa dunia imebadilika, ya zamani yamepita (uk. 36).  o Mila na desturi za jamii huwa na mafunzo ya kudumu. Sara aliishi wakati wa jana na  leo. Anatoa mafunzo kwa wanawe kuhusu utamaduni wa jana. Wakati Asna na  Neema wanamwambia kuwa hakuna tatizo lolote anapolala nyumbani kwa Neema  na Bunju, anadai kuwa mila zina mahali pake (uk. 36).  

o Kulingana na mila na desturi za kizazi cha jana, msichana akisha baleghe, sharti  aozwe (uk. 52).  

o Mila na tamaduni za kizazi cha jana kinawajenga wanaume kama watu wasioweza  kusaidia katika kazi za jikoni. Kazi zote za jikoni zimeachiwa wanawake. Hata mume anapomsaidia mkewe kazi hizo, anaonekana kushushwa hadhi yake (uk. 14).  o Inasemekana kuwa watu watamcheka na kusema amekaliwa (uk. 66).  

Elimu  

Suala la elimu limepewa kipaumbele katika tamthilia ya Bembea ya Maisha hasa na kizazi cha leo. Maudhui haya yamekuzwa na Yona, Mina, Lemi, Sara na watoto wa  Dina.  

Yona ni mwenye elimu kwa sababu alikuwa mwalimu. Yona anasema kuwa wakati  alipokuwa mwalimu, alikuwa akienda skuli wakati wa majira ya alfajiri, kiboko  mkononi. Anasema kuwa siku nzima ilikuwa kazi tu, jioni ni darasani tena.  Alipotoka shule, alikuwa akivifunga vitabu kwenye baiskeli kwenda kuvisahihisha  wikendi (uk. 62).  

Yona amesoma hadi Chuo kikuu. Alikuwa mtu wa kwanza pale kijijini kufuzu  kutoka chuoni.  

Mabinti wa Yona na Sara wanasawiriwa kama watoto walio na elimu.  

Elimu ya Neema inadhihirishwa tunapoambiwa kuwa amesoma hadi Chuo kikuu  na kuhitimu shahada mbili. Bunju anasema kuwa Asna amesoma hadi Chuo kikuu  alikohitimu digrii vilevile. Salome naye ameishi nyumbani kwa Bunju na Neema  huku akisoma Shule ya upili. 

Baadaye anafanikiwa kwenda Chuo kikuu alikopita na kupata first class.  Alibahatika kupata ufadhili wa kwenda kuendeleza masomo yake ng'ambo (uk.  28).  

Elimu imeonyeshwa kupitia watoto wa Neema na Bunju: Mina na Lemi. Mina  anasemekana kuwa anasomea Shule ya bweni. Lemi naye anakuza elimu kwa jinsi  anavyoshiriki katika kazi yake ya ziada baada ya kutoka shuleni. Bela anamweleza  Neema jinsi Lemi hujinengua anapocheza nyimbo za shuleni. Elimu imesawiriwa  kama nguzo ya ufanisi katika maisha ya leo. Wahusika waliosoma na kuhitimu  kama vile Yona, Neema na Sara wanafanikiwa kupata kazi na kuwa mwanga wa  kijijini.  

Migogoro  

a) Migogoro ni hali ya mvutano au kutoafikiana baina ya pande mbili au zaidi.  Migogoro katika tamthilia huzuka kwa sababu ya mambo mbalimbali  yanayokinzana. Katika tamthilia hii kuna migogoro ya kitamaduni kati ya  wanausasa na wanakizazi cha jana, migogoro katika ndoa, maisha na maendeleo ya  mjini na kijijini.  

b) Kuna mgogoro wa kitamaduni kati ya kizazi cha leo na kizazi cha jana  kinachoshikilia imani zilizopitwa na wakati. Kwa mfano, Asna anamwona babake  angali kijana na ana uwezo wa kutekeleza majukumu ya nyumbani kama vile kuteka maji kisimani. Wazo la Asna linaleta mvutano baina yake na mamake. Sara analiona  wazo hilo kama bovu na lisiloweza kutekelezwa na mumewe kwa sababu ya jinsi  wanajamii watakavyomchukulia. Sara anasema kuwa wanajamii watamshushia  hadhi na watamtazama kwa sini ya dharau (uk. 44-45).  

c) Utamaduni unazua mgogoro kati ya Asna na Sara. Kulingana na Sara, utamaduni wa  jamii unamtaka kila msichana aliyebaleghe aozwe.  

d) Asna anapinga utamaduni huo na kudai kuwa, hilo ni jambo lililopitwa na wakati.  Asna anadai kuwa msichana anaweza kuolewa au kukosa kuolewa. Na anapotaka  kuolewa, anaweza kuolewa kwa wakati autakao yeye bali Sio kwa wakati  wanaotaka wanajamii.  

e) Mgogoro unajitokeza baina ya mawazo ya Bunju kuhusu mila zinazowakataza  wazazi kulala nyumbani kwa mkwe na mawazo ya Neema, Asna na Bela. Neema  anapinga mawazo hayo na kusema kuwa mila hizo hazina thamani wala nafasi tena  katika dunia ya sasa (uk. 29). Asna naye anayapinga mawazo hayo kwa kusema  kuwa dunia imebadilika (uk. 36). Bela vilevile anapinga wazo hilo kwa kusema  kuwa hayo ni ya kale na kuwa watu wengi hawafuati mila hizo kwani ulimwengu  umebadilika (uk. 24).  

 

f) Kuna migogoro ambayo inazuka katika asasi ya ndoa. Ndoa ya Sara na Yona ni  yenye migogoro. Yona anasababisha mgogoro baina yake na Sara kwa kumchapa na  kumkosea hadhi Sara kwa kukosa mtoto wa kiume. 

g) Mgogoro huu unasababisha Sara kupatwa na maradhi ya moyo na kumfanya  mwanawe Asna kuona ndoa kama doa.  

h) Ndoa ya Bunju na Neema ina mvutano kuhusu suala la matumizi ya pesa na suala la  malezi ya mtoto wao Lemi. Bunju ana msimamo wake kuhusu majukumu yake kwa  familia yake na kusema gharama ya matibabu ya mamake Neema Sio jukumu lake.  Neema anahisi kuwa  

i) Bunju anaweza kumsaidia katika matibabu ya mama yake. Wawili hao wanavutana  kuhusu suala hilo. Wazo la Bunju linamfanya kumuona kama mkono birika na  asiyetaka kuwasaidia.  

j) Neema na Bunju wanavutana vilevile kuhusu suala la kumpeleka Lemi kwenda  kucheza na kuogelea na wenzake. Neema anamsihi Bunju ampeleke Lemi kujivinjari lakini Bunju anasema kuwa hawezi kwenda huko badala ya kwenda kuvuta riziki.  Isitoshe, anadai kuwa michezo hiyo hununuliwa si kama ya zamani (uk. 48).  

k) Bunju anasema kuwa Neema anapenda kukana na lazima abishe jambo ambalo  litamfanya kuonekana mbwa kasoro.  

l) Kuna mgogoro baina ya wanajamii na familia ya Yona. Mvutano unazuka wakati  ndoa ya Yona na Sara inakosa kujaliwa na mtoto.  

m) Wanajamii wanaikejeli na kuisuta ndoa hii na kumuita Yona gumba na Sara tasa.  Hata wanapopata watoto wasichana bado jamii inawasuta kwa kukosa mtoto wa  kiume.  

MBINU ZA LUGHA NA MBINU ZA KIMUUNDO  

Mwandishi wa tamthilia ya Bembeaya Maisha ametumia mbinu mbalimbali za lugha na  za kimuundo ili kuwasilisha dhamira na maudhui yake.  

Mbinu za lugha  

✔ Lugha ya kitamthilia ni lugha maalumu. Hii ni kwa sababu inatumika katika  utanzu wa kijukwaa. Jukwaa la uigizaji humpatia mwandishi fursa ya kutumia  lugha ambayo sharti iambatane na uigizaji. Vilevile, kuna lugha ya uigizaji  ambayo inaweza kuhusisha uteuzi wa maneno wenye urari kama katika ushairi.  

✔ Katika tamthilia ya Bembeaya Maisha, mwandishi ametumia lugha kwa njia  mwafaka ili kutekeleza malengo yake. Tamathali za usemi zimetumika kwa  wingi.  

 Taswira  

∙ Twasira ni dhana ambayo hutumia maneno ili kumchorea msomaji picha fulani  katika fikira au akili yake. Pia huitwa jazanda.  

∙ Inawezekana mwandishi kutumia taswira za kimaelezo au zile zilengazo hisi za  mwanadamu kama vile joto, mnuso, mguso na usikivu.  

 

Mifano  

🙓 Taswira inajitokeza kwenye maneno yaliyo kwenye mabano au yaliyoandikwa  katika hati ya kiitaliki. Maelezo hayo yanatuchorea picha akilini mwetu.  Yanatufahamisha na kutujulisha dhahiri wakati, mahali na matendo yanapofanyikia. 

🙓 Kwa mfano, katika onyesho la kwanza sehemu ya kwanza maneno yaliyo kwenye  mabano yanatuonyesha kwamba onyesho linafanyika wakati wa alasiri, mahali ni  nyumbani kwa Sara, tunaona Sara akichukua vidonge vya dawa na kuvimeza  

🙓 kabla ya kuketi kwenye kochi jipya. Tunaona namna ukuta wa nyumba ya Sara  umepambwa na picha za familia. Takriban maneno yote yaliyo kat:ika hati ya  kiitaliki yanatuchorea picha fulani akilini, hivyo yanajenga taswira.  

🙓 Taswira katika tamthilia hii pia imejidhihirisha kupitia kwa maneno yanayosemwa  na wahusika. Kupitia usemaji wa wahusika, msomaji anapata taswira fulani  kuhusiana na namna mhusika anavyozungumza. Kutokana na maneno yao, msomaji  hupata taswira sikivu ambayo inamdhihirishia toni au kiimbo anachotumia mhusika lengwa.  

🙓 Katika Onyesho I Sehemu I; mazungumzo kati ya Sara na Yona yanatuonyesha  taswira sikivu ya toni wanayotumia, Yona anatumia toni ya juu naye Sara anatumia  toni ya chini. Maneno Yao yanatuchorea picha akilini kuhusu wanavyozungumza.  Taswira ya aina hii ndio inayowezesha tamthilia kuigizwa jukwaani kwa kutumia  toni au kiimbo kinachofaa.  

🙓 Anwani ya tamthilia hii inatuchorea picha akilini. Neno bembea linarejelea kifaa  ambacho mara nyingi hutumika na watoto kuchezea. Kifaa hiki huenda juu na chini  na kurudi nyuma na mbele. Hivyo basi,  

🙓 BEMBEA YA MAISHA ni taswira fikirivu, msomaji anaposoma anwani hii anapata  mawazo mengi kuhusu maisha ambayo anayalinganisha na bembea. Msomaji  anatarajia kupatana na maisha ambayo yana panda shuka au ambayo yanayumbisha anaposoma tamthilia nzima. Hali hii inadhihirika wazi kwa kuwa anwani Bembea ya Maisha imejidhihirisha katika maelezo na matendo ya wahusika katika tamthilia  nzima.  

Mifano ya taswira inayojitokeza katika dondoo  

i) ...Miaka inaposonga mnatuona...kama..kama vile tambara bovu. Tambara lisilomjia  hata mpiga deki akilini (uk. 4). Maneno haya yanatumiwa na Yona yakielekezewa  mkewe. Maneno haya yanaonyesha namna wanaume hawana umuhimu wowote  kwa wanawake katika jamii ya tamthilia hii.  

ii) ...Wewe unaona rangi ya mwisho wa kinachoelea. Kabla kielee kimepigwa shoka,  kimeonja misumeno aina aina, kimetambaliwa na randa, kimestahimili makali ya  patasi na kupapaswa na mikwaruzo ya msasa (uk. 10). Haya ni maneno ya Dina  akimweleza Kiwa kuhusu maisha ya mabinti wa Yona na Sara. Maneno haya  yanatujengea taswira ya maono. Msomaji anaposoma maelezo haya anaona picha  ya watu walioishi kuteseka, kunyanyaswa na kwa jumla watu walioishi maisha  magumu sana kisha kufanikiwa baadaye.  

 

iii) ...Nilikuwa kimbaumbau mwiko wa pilau. Upepo mchache tu ungeniyumbisha  kamajani kavu wakati wa kipupwe (uk. 10). Haya ni maneno ya Sara akimweleza  Dina. Maneno haya yanatuonyesha taswira ya maono. Tunaona namna mwili wa  Sara ulikuwa umedhoofika na afya yake kuzorota kwa kukondeana kama ngonda  hadi kufikia kiwango cha kupeperushwa na upepo.  

iv) ...Mkulima hodari libasi yake huwa imechakaa na kuchoka lakini moyoni anabaki  kama theluji kwa kutosheka na tija ya sulubu zake. Huwezi kumlinganisha na  mkulima wa nguo safi zilizopigwa pasi zikanyooka (uk. 18). Haya ni maneno ya  Sara ya kumpongeza Neema kwa juhudi zake za kujiendeleza kimaisha.  Analinganisha hali hii na ya mkulima ambaye amelazimika kufanya kazi ngumu  shambani na kupata vuno zuri. Ili afanikiwe sharti nguo zake zichafuliwe na  udongo na mchanga. Kama angaliogopa kuchafuka basi mkulima asingelifanikiwa.  

v) ...Mwanangu usitake kuhoji alacho kuku. Utachafukiwa roho umchukie kuku bure.  Wala usitake kujua asali ameitengenezea nini nyuki. Hutaila.  

Maadamyameshakujayapokee (uk. 20). Kupitia maneno haya, Sara anampatia  Neema moyo ili ajikaze na kumvumilia mumewe kwa kupuuza udhaifu wake  kwani asipofanya hayo ndoa yake na Bunju inaweza kuingia doa.  

vi) ... Bembea inapolika na kukatika haiwi mwisho wa mchezo. Huungwa na mchezo  kuanza tena (uk. 21). Sara analinganisha mchezo wa watoto wa kubembea na  maingiliano ya ndoa. Mchezo wa bembea humalizika kwa sababu bembea  imekatika na uhusiano wa ndoa hutatizika wanandoa wanapokosa kuvumiliana.  

vii).... Ni kama mti mchanga kwenye chaka la miti mikubwa mirefu. Unaishi kutapia  hewa na jua. Unajitahidi kutoa Shingo kila wakati kuung'ang'ania mwanga huo.  (uk. 26) Haya ni maneno ya Neema akimweleza Bela namna watu wa tabaka la  chini hulazimika kufanya bidii ili kujinyanyua kutokana na mnaso wa umaskini.  Hali hii inalinganishwa na jinsi miti michanga inavyong'an

Misemo  

Misemo ni aina ya semi fupi zenye ukweli ambazo hutumiwa kuelezea mambo yenye  kuafiki ukweli huo. Mwandishi ametumia mifano kadhaa ya misemo katika tamthilia hii. 

Mifano  

a) Kutupigajeki (uk. 3) - Kumpa mtu msaada au kusaidia.  

b) Kuadimika kama wali wa daku (uk. 5) - Ni kutoonekana kwa muda mrefu sana.  c) Kufanya nongwa (uk. 12) - Kusongwa na moyo kutokana na jambo linaloudhi.  d) Kila limfikalo mwanadamu ni mpango wa Manani (uk. 12) - Imani kuhusu  

majaaliwa ya kwamba tunayokutana nayo ni mpango wa Mwenyezi Mungu.  e) Kupiga makasia chombo kinapopungukiwa na upepo (uk. 14) Kutoa msaada  wakati hali ngumu inapomkabili mwenzako.  

f) Kichwa kimeudara mto (uk. 1) - Kichwa kimelala juu ya mto.  

g) Tiwa vinywani (uk. 6) - Semwa sana na watu.  

 

h) Bongo za sumaku (uk. 7) - Bongo zinazoweza kushika mambo kwa urahisi.  i) Sisimkwa na malaika (uk. 12) - Kuwa na wasiwasi.  

j) Nisiyatie machungu moyoni (uk. 12) - Nisihuzunike, nisiwe na wasiwasi.  k) Watoto ni baraka (uk. 18) - Watoto ni majaliwa ya Mwenyezi Mungu.  l) Fungulia milangoya heri (uk. 18) - Achilia baraka.  

m) Ingiajakamoyo (uk. 44) - Patwa na wasiwasi.  

n) Ponza roho (uk. 44) - Jiingize katika matatizo.  

o) Ana bidiiya mchwa (uk. 45) - Bidii kubwa.  

p) Kutokuwa na kabaya ulimi (uk. 48) Kutojizuia, kusema sana na kila wakati.  q) Kuwa chiniya amri (uk. 49) - Kuwa mtiifu.  

r) Ujana ni moshi (uk. 52) - Ujana ni sawa na moshi ambao ukienda haurudi.  s) Ndoa ni mtihani mkubwa (uk. 53) - Ndoa ina matatizo mengi; inahitaji hekima.  

Nahau  

Nahau ni aina ya semi ambazo huundwa kwa fungu la maneno ya kawaida yanayozua  maana tofauti na ile ya maneno hayo. Nahau ni maneno ya busara ambayo hutumiwa  kueleza kitu kutokana na mifano katika maisha. Ni bayana kwamba nahau hutokana na  mazingira ya watumiaji wa lugha husika. Nahau hutumiwa kupamba lugha na kupunza  ukali wa maneno.  

Mifano  

1) Kutupa jogoo na mti wake (uk. 3) - Inamaanisha kuachana na jambo kabisa. Sara  anarejelea jinsi ambavyo baadhi ya wasichana wanavyowasahau ndugu zao  wanapoolewa.  

2) Bahatiya mtende (uk. 3) - Ni kubahatika sana kwa njia isiyotarajiwa.  3) Kushindana na ng'onda (uk. 5) - Kukonda sana.  

4) Kikapu cha mama kimejaa ndago (uk. 6) - Usemi unaoashiria mtu aliyefanikiwa.  Usemi huu unamrejelea Sara ambaye alikuwa na uhitaji siku za nyuma lakini sasa  bintize wanamfaa kwa hali na mali.  

5) Maji kuzidi unga (uk. 11) - Hali kuwa tatizi au ngumu kukabiliana nayo.  6) Utakuwa unajivulia nguo (uk. 14) - Utakuwa unajiaibisha.  

7) Nyotayajaha (uk. 19) - Bahati.  

8) Tumeyaacha maji ya mbizi tukaingia maji ya mbuzi (uk. 20) Tumetoka kwenye hali  ngumu na sasa tumeingia kwenye hali nafuu.  

9) Taaridhi isiyo kifani (uk. 24) - Udadisi; hali ya kuuliza uliza au kuchunguza mambo.  10) Bora punda afe mzigo ufike (uk. 27) - Kutomjali mfanyakazi bora tu kazi  ifanyike. Hata anayeifanya akidhurika Sio hoja.  

11) Fanya ajizi (uk. 1) - Legea, kuwa mvivu, zembea. Zika katika giza la kina cha  moyo (uk. 7) - Nyamazia jambo au fanya kuwa siri.  

12) Angukiwa na nyotayajaha (uk. 19) - Bahatika.  

13) Piga kalamu (uk. 19) - Achisha kazi.  

14) Walimwengu sasa wanavaa sare moja (uk. 24) - Watu wamebadilika;  wameachana na ya kitambo na wanafuata ya sasa. Akili za madongo kuinama (uk.  23) - Akili hafifu zisizo imara.  

15) Mchele umeingia mchanga (uk. 26) - Mambo yameharibika.  16) Poa moto (uk. 26) - Tuliza hasira; kuwa mpole.  

17) Bunju ni mkono wa birika (uk. 33) - Ni mchoyo.  

18) Chombo kingezama (uk. 62) - Mambo yangeharibika.  

19) Kujipiga kifua (uk. 63) - Kujigamba.  

20) Kata shauri (uk. 70) - Amua.  

21) Sikuwa na picha nzima (uk. 74) - Sikuwa na ufahamu wa kutosha.   Mbinu ya majazi  

Majazi ni mbinu ambayo mwandishi hutumia kuwapa wahusika majina kulingana na  tabia zao. Mbinu hii inadhihirika kupitia kwa wahusika kama vile:  

🙓 Bunju - jina Bunju ni la kimajazi. Bunju alipewa jina hili lililolinganishwa na  mnyama mwenye sumu lakini sumu hiyo huondoka baada ya kusafishwa. Bunju  ana tabia mbaya inayolinganishwa na sumu ya mnyama huyo. Kwa mfano,  alionekana kuwa na ukali kwa mambo ya kusaidia Neema katika matibabu ya  mama mkwe (Sara). Baada ya kushawishiwa kwa muda na Neema, ukali huo  unamwondoka na kumweleza Neema kwamba atamsaidia kulipa gharama ya  matibabu ya mama yake (uk. 40). Anamwambia atampiga jeki.  

🙓 Neema - Neema ni jina la kimajazi. Neno neema lina maana ya kufanikiwa au  kustawi. Mwandishi amempa Neema jina hili kutokana na sifa za kustawi na  kufanikiwa maishani. Neema amefanikiwa kusoma hadi Chuo kikuu na kustawi  kwa digrii mbili, amefanikiwa kupata kazi nzuri, amefanikiwa kupata mume  anayemjali na kushughulikia maisha ya familia yake na pia amefanikiwa  kuwalipia karo dada zake hadi Chuo kikuu. Kwa kifupi, mhusika Neema  amefanikiwa kwa kiasi kikubwa maishani.  

🙓 Sara - mhusika Sara amepewa jina hili kutokana na namna alivyosemwa na  wanajamii. Neno sara lina maana ya kutapakazwa au kuenezwa kila mahali. Jina  la Sara lilienezwa na wanajamii kila mahali. Alisemwa sana na kutukanwa kwa  kuwa hakuwa na watoto wa kiume (uk. 13). Alisemwa kotekote ikiwemo  makanisani na magengeni. Kwa sababu hii mwandishi akampa mhusika huyo  jina, Sara.  

Lakabu  

∙ Lakabu ni mbinu ambayo mwandishi hutumia kuwapa wahusika majina mbali  na majina yao halisi. Lakabu huwa ni jina la kupanga au jina la kutania. Mhusika  ametumia mbinu hii kuwarejelea wahusika kama vile:  

∙ Kalasinga - hili ni jina alilojipa baba yake Yona. Alijipa jina hili kwa kuwa  alikuwa Mwafrika wa kwanza kufanya kazi kwa Mhindi. Mhusika huyo alijifunza  

 

Kihindi na kufanikiwa kukimudu vizuri baadaye akajipa jina Kalasinga.  Kalasinga si jina lake halisi ila ni jina la kupanga.  

Tasfida  

Tasfida ni matumizi ya maneno yanayoficha ukali wa hali fulani. Mwandishi anatumia  mbinu hii kupitia kwa mifano ifuatayo:  

🙓 Sara: Hata nikiitwa nitaondoka nikiwa nimeridhika (uk.13). Haya ni maneno ya  Sara akirejelea ufanisi wa watoto wake ambao walikuwa wanachekwa na  majirani kutokana na fikra kuwa hawawezi kufaulu kwa sababu ya uhitaji wa  wazazi wao. Sara anamaanisha kwamba hata  

🙓 akiaga dunia atakuwa ametekeleza azimio lake la kuwasaidia watoto wake  kufaulu maishani.  

🙓 Bunju: Unataka nifurahi ghaya wakati huna kamba ya ulimi (uk. 48). Haya ni  maneno ya Bunju kwa Neema. Bunju anatumia tafsida kwa kutumia neno"kamba ya ulimi," kuficha ukali fulani. Maneno haya yanamaanisha kwamba Neema  anaongea sana au anaropokwa na maneno.  

🙓 Dina: wewe umekua ukampata Yona kipenzi cha maji (uk. 10). Kipenzi cha maji  ni maneno yenye maana ya mtu anayependa pombe; mievi  

🙓 Sara: watt/ walituona masikini wa watoto. Maskini wa kizazi (uk. 55).  kupindukia. Maneno haya yametumiwa kurejelea mtu asiye na uwezo wa kupata mtoto, badala ya kutumia maneno ya moja kwa moja na makali kama vile gumba au tasa.  

Kuchanganya ndimi  

Kuchanganya ndimi ni mbinu inayotumiwa na mwandishi kuonyesha hali ya  kuzungumza lugha mbili au zaidi kwa pamoja. Mwandishi wa tamthilia hii ametumia  mbinu hii katika uandishi wake kama ishara ya maudhui ya elimu na pia kusawiri hadhi ya wahusika fulani kama walioelimika.  

Mifano:  

1) Culture shock (uk. 46) - Usemi huu unamaanisha hali ya kushangazwa na  mienendo ya watu ambao wana utamaduni tofauti au mazoea tofauti na yale  ambayo mtu aliyatarajia.  

2) Homework (uk. 40). Asna anasema Lemi amempa homework. Hii ina maana  kuwa amempa kazi ya ziada. Pia ukurasa 49, Bunju anasema kuwa "ninamsaidia  kufanya homework".  

3) Boarding school (uk. 27). Usemi huu una maana ya shule ya bweni.  4) First class(uk. 28). Usemi huu unamaanisha kiwango cha juu zaidi cha kupita  mtihani wa Chuo kikuu.  

5) Flying doctors (uk. 41). Usemi huu unamaanisha madaktari ambao husafirishwa  kwa ndege ili kufika haraka mahali penye wagonjwa mahututi.  

 

6) My foot (uk. 26). Mwandishi ametumia usemi huu kukejeli. Bunju anatumia  usemi huu kumkejeli mke wake Neema. Ni usemi unaotumiwa katika jamii ya  kisasa na vijana kwa lengo la kutupilia mbali mawazo ya watu wengine.  

7) Hii Servant Quarter inanitosha (uk. 31). Asna anatumia neno servant quarter  kurejelea chumba anamoishi jijini. Chumba cha aina hii aghalabu hutumiwa na  wafanyakazi wadogo kwenye boma la mwajiri wao. Kwa hivyo, iwapo Asna  anaishi mtaa wa kifahari, hana nyumba ya kifahari huko bali anaishi katika  chumba kidogo tu.  

8) I wish wangeelewa (uk. 72). Neema anatumia maneno I wish kuonyesha  matamanio yake kwa wale wanaopewa kibarua kujua kuwa waajiri wao  wanapitia magumu ili kupata mali kidogo waliyonayo.  

9) Sharp (uk. 73). Katika muktadha wa matumizi usemi huu una maana ya kuelewa  mambo kwa upesi au kwa haraka.  

10)Mum (uk. 47). Lemi anatumia jina hili kumwita mama yake. Mum ni jina la  Kiingereza linalomaanisha mama.  

11)Kesho una time umpeleke huyu out? (uk. 48). Katika muktadha wa matumizi,  neno out lina maana ya 'ziara'. Yaani kwenda kuburudika na kujivinjari. Lemi  alitaka kupelekwa out wakacheze na kuogelea pamoja na watoto wengine. Nalo  neno time limetumiwa kuonyesha 'nafasi'.  

12)Tomboy (uk. 52). Hii ina maana ya msichana anayeishi na kutenda mambo kama  mvulana.  

 Kubadili msimbo  

Hii ni mbinu ya kubadilisha lugha wakati wa mazungumzo na kuanza kutumia lugha  nyingine tofauti na ile ya kwanza. Mwandishi ametumia mbinu hii katika tamthilia  kuonyesha hekima au elimu..  

Mfano;  

If wishes were horses beggers would ride (uk. 72). Maneno haya yalisemwa na Yona  kwa Neema. Mhusika Yona anabadili msimbo kutoka kwa lugha ya Kiswahili hadi lugha  ya Kiingereza kwa kutunga sentensi nzima. Ni kauli inayodhihirisha majuto na nia ya  mabadiliko kwa upande wa Yona.  

Maswali ya balagha  

Hii ni njia ya usemi ambayo hutumia maswali yaliyokusudiwa kusababisha athari fulani bila kutarajia majibu.  

Mtindo huu umetumiwa na Sara anayeuliza:  

(Kwa ukali.) Hivi mtoto una akili wewe? Babako aende kuteka maji  kisimani? Wazee wenziwe watamwonaje? Kijiji kitasema nini? Kwamba 

amesomesha watoto ambao wameniweka jijini ili baba yao ataabike2 hiyo ndiyo  heshima?(uk. 44)  

Sara alikusudia kuonyesha hisia zake kuhusu kuendelea kukaa kwake mjini na  kumsababishia mumewe izara. Usemi huu pia unaendeleza maudhui ya utamaduni,  migogoro, na nafasi ya mwanamke katika jamii pamoja na kusawiri sifa za Sara.  

Mbinu hii imetumika pia katika mazungumzo nafsia ya Neema (uk. 41). Anajiuliza: Leo  tungekuwa wapi bila Bunju? ...Mtu huyo atakosaje kuwa zawadi kwako? Maswali haya  yanadhihirisha mabadiliko katika hisia za Neema juu ya mumewe Bunju. Anaanza  kumthamini zaidi. 

Utohozi  

Utohozi ni mbinu ya kubadili maumbo ya maneno ya lugha moja na kuyafanya  yachukue muundo wa lugha nyingine. Mwandishi ametumia majina ya kutoholewa  kutoka lugha ya Kimombo hadi lugha ya Kiswahili. Mifano  

🙓 Hospitali (uk. 51) - neno hili limetoholewa kutoka kwa neno la Kiingereza  hospital.  

🙓 Familia - limetokana na neno la Kiingerezafamily.  

🙓 Skuli - limetoholewa kutoka neno la Kiingereza school.  

🙓 Presha (uk. 11) - limetoholewa kutoka neno la Kiingereza pressure.  🙓 Daktari (uk. 12) - limetoholewa kutoka neno la Kiingereza doctor.  🙓 Afisini (uk. 27) - limetokana na neno la Kiingereza office.  

🙓 Kliniki (uk. 14) - neno hili limetokana na neno la Kiingereza clinic.  🙓 Hoteli (uk. 42) - jina hili limetoholewa kutoka kwa neno la Kiingereza hotel.  🙓 Rekodi (uk. 73) - neno lililotoholewa kutoka neno la Kiingereza record.  

Tashbihi  

Huu ni usemi wa ulinganisho au ufananisho wa vitu viwili au zaidi kwa kutumia  maneno ya ulinganishi: kama vile, kama, mithili ya, mfano wa na kadhalika.  

Mifano  

1) Tafunwa kama chingamu (uk. 6); kusemwa sana na watu.  

2) Kutuona kama tambara bovu (uk. 4); ni kuonekana vibaya au kitu kisicho na  thamani.  

3) Hayayalikuwa kama vishindo vya mashua na Sisi kama bahari (uk. 56); maana  ya tashibihi hii kulingana na matumizi ya muktadha ni kwamba matatizo ya  maisha yao yanafananishwa na hali ya mashua kupita kwenye bahari na  kwamba walistahimili na kufaulu..  

4) Tunaendeshwa kama tiara (uk. 23); kuendeshwa hivihivi. Kazi kama safari ya  ahera (uk. 23); kazi ambayo inachosha; isiyokamilika.  

5) Ni wazi kama mchana (uk. 3) - jambo lisilofichika, lisilo siri.  

6) Mwili mzima mfano wa bua (uk. 4) mwepesi mno. - mwili hauna nguvu, ni  

 

7) Ni kama msafiri katikajangwa (uk. 7) - mtu mwenye kiu au tamaa ya kupata kitu  fulani.  

8) Mwanadamu sawa na tumbo, hakinai (uk. 8) - mwanadamu hatosheki.  9) ponyoka kama maji kwenye viganja (uk. 10) - jambo lisiloweza kuzuiwa.  10) Upepo ungeniyumbisha kamajani kavu (uk. 12) - upepo ungempeleka  kokote ufanyavyo majani makavu.  

11) Maisha yamekuwa mfano wa gurudumu kwenye gari la masafa marefu  (uk. 23). Hata gurudumu likichoka halina hiari. Litaenda tu namna  litakavyovingirishwa. Watu hawana chaguo ila kuendelea na maisha yajavyo.  

12) Kujisikia kama abiria kwenye gari liendalo kasi (uk. 29) - kuwa na  wasiwasi; kutotulia.  

13) Konda kama ng'onda (uk. 32) - konda kupindukia. Mwoga kama kunguru  (uk. 34) - mwoga sana.  

14) Safi kama pamba (uk. 35) — bila doa, uzuri uliokamilika. Hospitali za  kijijini ni kama seli (uk. 42) - hali yake ni mbovu.  

15) Watoto wa siku hizi wanakua mithili ya mchicha (uk. 43) wanakua kwa  kasi.  

16) Ana moyo kamajiwe (uk. 45) - ana moyo mgumu; si mwepesi wa kutoa; ni mchoyo.  

17) Kuteleza kama sabuniya povujingi (uk. 56) - kushindwa kumudu hali  yake.  

Methali 

Methali ni aina ya semi ambayo huwa na muundo maalumu. Hueleza ukweli fulani  wenye maana pana na unaoweza kufasiriwa kwa njia mbalimbali.  

Methali hukusudia kuonya, kuelekeza, kuadhibu, kusuta, kulaumu, kushauri na  kadhalika. Methali huwa imebeba maana pana kuliko maneno yenyewe.  

Tamthilia ya Bembea ya Maisha imetumia mbinu ya methali kwa wingi.  Mifano:  

1) Mungu hamwachi mja wake (uk. 8).  

2) Kigumba kwa nguruwe kwa binadamu ki uchungu (uk. 63).  

3) Baada ya dhiki faraja (uk. 6).  

4) Njia haimuagulii msafiri (uk. 6).  

5) Binadamu mchoyo kwa lake lakini mkarimu ajabu kwa la mwenziwe (uk. 5).  6) Mlango mmoja ukifunga, macho huiona mingine mingi (uk. 56).  7) Mwacha mila ni mtumwa (uk. 58).  

8) Mgala muue na haki yake mpe (uk. 66).  

9) Hakuna kizuri kijacho kwa urahisi (uk. 67).  

10) Kutoa ni moyo, usambe ni utajiri (uk. 2)  

11) Mtu hujikuna ajipatapo (uk. 2)  

12) Mungu si Athumani (uk. 10)  

13) Mungu hamtupi mja wake (uk. 10)  

14) Leo kwangu kesho kwal<0 (uk. 11)  

15) Mungu hamwachi mja wake (uk. 11)  

16) Safari ya kesho huungwa leo (uk. 16)  

17) Mrina haogopi nyuki (uk. 18)  

18) Papo kwa hapo kamba hukata jiwe (uk. 21)  

19) Mwana wa yungwi hulewa (uk. 21)  

20) Kipendacho roho hula nyama mbichi (uk. 21)  

21) Ya kale hayanuki (uk. 24)  

22) Mapema ina sudi (uk. 25)  

23) Afikaye kisimani mapema hunywa maji maenge (uk. 25)  24) Samaki hukunjwa angali mbichi (uk. 26)  

25) Msafiri kafiri angawa tajiri (uk. 31)  

26) Mwindaji huwa mwindwa (uk. 32)  

27) Ng'ombe halemewi na nunduye (uk. 35)  

28) Mali ya bahili huliwa na mchwa (uk. 45)  

29) Mgala muue na haki umpe (uk. 66)  

Methali katika tamthilia ya Bembeaya Maisha zimetumika kutekeleza yafuatayo:  

🙓 Kupamba lugha na kuipa mvuto wa kisanaa.  

🙓 Kuendeleza maudhui na dhamira ya mwandishi, hasa kuhusu suala Zima la  bembea ya maisha.  

Sitiari  

Ni mbinu ya lugha inayotumia ulinganisho wa moja kwa moja wa kitu na kingine. Kitu  kimoja husemwa kuwa kingine. Mifano ya sitiari katika tamthilia ya Bembea ya Maisha.  

1) Mbegu ipandwayo haina budi kuzaa na izaapo mazao yake huvunwa. Mtu  huitakasa sahani yake akijua itamfaa tena. (uk. 1-2). Yona analinganisha wanawe (Asna na Neema) na mbegu, mazao yake, na mavuno. Pia, anawalinganisha na  sahani ambayo aliitakasa imfae.  

2) Katika uk. 2, Sara anasema kuwa Neema ana 'mzigo' wa familia yake. Mzigo  umetumiwa kama sitiari ya majukumu mengi au mazito.  

3) Vilevile, kwenye uk. 2, Yona anasema kuwa fimbo ya mzee hurithiwa na mtoto  wa kwanza. Fimbo ni sitiari ya nafasi ya mzee katika familia.  

4) Ukurasa wa 3, Sara anasema kwamba wachapakazi hodari ni njozi iliyopotea. Hii ina maana kuwa hawapatikani.  

5) Mimi mzigo (uk. 4) - mtu ambaye ni tatizo kwa jamaa zake, anayetekelezewa  majukumu yake yote.  

6) Amekuwa na kimo cha sindano (uk. 5) - amekuwa mwembamba sana.  7) Neema ni chuma cha reli (uk. 6) - Neema ana nguvu za kustahimili changamoto  za maisha.  

 

8) Katika uk. 8, mvua ya baraka iliwanyea Yona na Sara. Mvua ya baraka ni sitiari  ya watoto ambao Yona na Sara walibarikiwa kuwapata.  

9) Dina anaeleza kuwa watu walimtaka Yona kutafuta mtoto wa kiume ili "utambi  wa ukoo wake usizime" (uk. 10). Utambi wa ukoo ni sitiari ya kizazi cha ukoo.  10) Ukurasa wa 11, dunia ni nyumba ya mitihani. Hii ina maana kuwa dunia  ni mahali pa changamoto nyingi.  

11) Sara anasema kuwa alipoanza kuugua alikuwa kimbaumbau mwiko wa  pilau (uk. 12) - hii ina maana kuwa alikuwa mwembamba na mithili ya mwiko  wa kupikia pilau.  

12) Safari hii ni maji ya mbizi (uk. 16) - safari ni ndefu Maisha ya siku hizi si  maji ya kunywa (uk. 23). Maisha si rahisi au mepesi.  

13) Mamangu mzazi ni mboni ya jicho kwetu (uk. 30) - mama mzazi ni  mwangalizi wao.  

14) Nyumbani, hiki ni kizimba cha kuku (uk. 31) - ni chumba kidogo na duni.  15) Maisha ni mshumaa usio mkesha (uk. 32) maisha ni mafupi na hayapo  daima.  

16) Sara na Bunju ni chanda na pete (uk. 36) - wanalingana katika maoni yao,  ni wamoja.  

17) Mifuko inazidi kuwa king'onda (uk. 41) - inaendelea kuishiwa  18) Akili za Yona zinatajwa kuwa sumaku (uk. 43) - zinashika mambo haraka. 19) Nina jeshi lake (uk. 46) - nina watoto wake.  

20) Bunju anamweleza Neema kuwa kuwa yeye (Bunju) ni kichwa na Neema  ni shingo (uk. 49). Hii ina maana kuwa Bunju ndiye kiongozi wa nyumba naye  Neema ni msaidizi wake.  

21) Ujana ni moshi (uk. 52) - ujana ni kitu kinachopita na kikienda hakirudi.  22) Ndoa ni mtihani mkubwa sana (uk. 53) ndoa ina majaribu mengi.  23) Luka anamrejelea Neema kama 'simba wa kike anayenguruma' (uk. 61). -  

hii ina maana kuwa Neema ana sauti, usemi au hadhi sawa na ya mtoto wa  kiume.  

24) Watoto walikuwa nyota ya jaha (uk. 61) — ina maana kuwa watoto wa  Sara na Yona walikuwa bahati kubwa kwao.  

25) Mwanamume ni mto wa kifuu (uk. 67) - ina maana kuwa mwanamume  amesawiriwa kama mtu hatari.  

26) Sasa rudini mzalishe mbegu nzuri (uk. 68) - wawasaidie watoto wengine  kukua vyema kama wao; wawe mfano kwa wengine.  

27) Shikeni usukani muwe marubani wa kweli ili ndege ipae angani (uk. 68) -  chukueni nafasi ya kuleta maendeleo kijijini.  

Tashihisi  

Tashihisi ni mbinu ya mwandishi kuvipa viumbe visivyo na uhai sifa za uhai au za  kibinadamu. Pia huitwa uhuishi.  

🙓 Katika uk. 5, Kiwa anasema kuwa mvua yenyewe imefanya ugeni. Kiwa  analinganisha mvua na mgeni, na hivyo kuipa mvua sifa za uhai.  

🙓 Katika uk. 6, Dina anasema kuwa maradhi yamemgeuza Sara kuwa ngoma.  Katika mfano huu, maradhi yamesawiriwa kuwa yenye uwezo wa kumpiga Sara  kama vile mtu anavyopiga ngoma.  

🙓 Katika uk. 9, Dina anamweleza Kiwa kuwa "dunia mwanangu imetufunza Sisi  wazee wenu". Katika mfano huu, dunia imepewa uwezo wa kutoa mafunzo. Hii  ina maana kuwa matukio mbalimbali duniani yana uwezo mkubwa juu ya  maisha ya mwanadamu.  

🙓 Tashihisi pia imetumika katika uk. 38. Neema analalamika kuhusu maradhi  yasiyosikia dawa. Anasema, maradhi "yakitaka huzichezea dawa mwajificho.  Dawa zikiingilia huku, maradhi hutokezea pale, hali pesa zinakwenda, shughuli  zinasimama". Vitu hivi vitatu: maradhi,pesa na shughuli vinasawiriwa kuwa na  uwezo fulani ambapo maradhi yanazidi uwezo wa vyote viwili.  

🙓 Vilevile, tashihisi imetumika katika uk. 39 ambapo Bunju anamwambia Neema  kuwa "chumba chenyewe kinajisemea". Hii ni baada ya Bunju kufika nyumbani  kwake na kupendezwa na uzuri wa chumba hicho. Mfano huu una athari ya  kusisitiza uzuri wa chumba hicho usiofichika.  

🙓 Mbinu hii pia imetumika katika uk. 56 ambapo Sara anasema kuwa agongo  liliyamega maadili" ya Yona kimyakimya na taratibu uwajibikaji wake ukawa  umemponyoka. Gongo ni aina ya pombe kali.  

🙓 Mwandishi wa Bembea ya Maisha ameisawiri pombe hii kuwa na uwezo juu ya  mwenendo wa maisha ya mtu na kuweza kumdhuru mtu huyo.  

🙓 Vilevile, katika uk. 62, Beni anasema kuwa Yona alikuwa mwalimu mwenye bidii kabla "tembo kunyoosha mikono yake na kumdaka". Mfano huu, sawa na ule  uliotangulia hapo juu, unadhihirisha uwezo mkubwa wa pombe kumteka na  kumyumbisha mtu.  

Mbinu za kishairi  

Mbinu za kishairi ni sehemu muhimu ya matumizi ya lugha katika tungo za kitamthilia.  Miongoni mwa mbinu hizo muhimu ni takriri.  

Takriri 

Takriri ni urudiaji wa sauti, silabi, neno au sentensi za namna moja zinazofuatana kwa  karibu. Takriri hupamba lugha katika fasihi na pia kuvuta nadhari ya msomaji au  msikilizaji.  

Mwandishi wa tamthilia ya Bembeaya Maisha ametumia mbinu ya takriri katika kazi  yake. Mifano:  

🕮 Sara: ... Ulikuwa umenila kiasi cha kuniacha chicha. (uk. 2).  

🕮 Kiwa: Dunia ya leo haithamini kimo, inathamini akili. Haitaki kututumua misuli,  inataka tambo la fikira. (uk. 5).  

🕮 Dina: Dunia hii sasa tunaishi katika hofu. Tunahofu hata tusichokifahamu. (uk.  9).  

🕮 Dina: Wewe unaona rangi, tena rangi ya mwisho wa kinachoelea. Kabla kielee  kimepigwa shoka, kimeonja misumeno ainaaina, kimetambaliwa na randa,  kimestahimili makali ya patasi, na kukapaswa na mikwaruzo ya msasa. (uk. 10).  

🕮 Sara: Wewe unajua yote yaliyosemwa, hadharani na faraghani. Si makanisani, si  magengeni. (uk. 13). Sara: Tena hodari wa misemo na nahau. Wala hawana  simile  

🕮 kutuloweka kwenye misemo na nahau zao. Hawana simile mwanangu!  🕮 Sara: Tumeyaacha maji ya mbizi na kuingia kwenye maji ya mbuzi. (uk. 20).  🕮 Neerna: Kikijanjaruka hakitakuwa na budi ila kurauka. (uk. 25).  🕮 Neema: Usingepikika, usingelika. (ul<. 41).  

🕮 Neema: Mwenyewe huyo analipia kila kitu. Ninakwambia kila kitu! (uk. 41).  🕮 Asna: Ndoa imeyatia doa maisha yako. (uk. 53).  

🕮 Sara: Hizo juu-chini chini-juu ndizo utamu wake. (uk. 54).  

🕮 Asna: Elimu ni muhimu mama. (uk. 55).  

🕮 Sara: Mungu hakupi yote. Akikupa hiki, anakunyima kile.  

🕮 Akikupa yote yatakushinda. (uk. 55). Sara: Watu walituona maskini wa watoto.  Maskini wa kizazi. (uk. 55).  

🕮 Sara: Wakatulaumu na kutusema bila simile. Bila simile! (uk. 56).  🕮 Yona: Malezi yameachiwa yaya. Nyumba ni ya yaya. (uk. 59).  

🕮 (xviii) Yona: Asubuhi niko skuli majira ya alfajiri, kiboko mkononi...  🕮 Jioni darasani tena, kiboko mkononi. (uk. 62).  

🕮 Yona: Nilishindwa kuingia kazini kila siku. Nilishindwa kuishi bila kulewa. (uk.  62).  

🕮 Yona: Yabarikiwe mashamba yetu.  

🕮 Beni: Ibarikiwe mimea yetu.  

🕮 Luka: Vibarikiwe vizazi vyetu. (uk. 64).  

🕮 Neema: Kwenye hujuma na kuchimbana, kwenye ugomvi na mivutano, kwenye  chuki na uhasama wa kitoto, kwenye tembo na gumzo lisiloisha, penye uchimvi  na kusutana (uk.65).  

🕮 Sara: Anza polepole. Anza na baba yenu. Badala ya kumkabili, mshawishi.  Atakuelewa. Akikuelewa atauendeleza ujumbe. (uk. 69).  

🕮 Yona: Siku zangu za uzeeni lazima nizitumie kumwangalia mke wangu mgonjwa. Lazima nimshukuru kwa vitendo kwa jinsi alivyojitolea kuijenga familia yetu.  Kwaheri pombe. Buriani. (uk. 70).  

Ishara na taashira  

Ishara katika fasihi hutumiwa kurejelea kitendo, hali au kitu kinachodokeza au  kuonyesha dalili ya kitu kingine. Nayo taashira ni alama mahususi ambazo huhusishwa  na hali fulani katika jamii.  

 

1) Katika uk. 1, Yona analalamika kuwa nyumba haifuki moshi. Kufuka kwa moshi  ni ishara ya upishi. Kutokuwepo kwa moshi ni ishara na pia taashira kuwa  hakuna kinachopikwa.  

2) Mwangaza hafifu unaotokana na taa ya sola katika chumba cha Asna mjini ni  ishara ya maisha ya Asna. Mwangaza huu hafifu unaashiria kuwa ingawa Asna  anaona anaishi maisha mazuri na katika mtaa wa kifahari, mazingira anamoishi  si mazuri sana. Uzuri wake ni hafifu. Chumbani humo hamna vitu vya thamani  vinavyoendana na maisha ya kifahari. Ishara hii ni kama kejeli kwa maisha  anayoishi Asna.  

3) Katika uk. 6, Dina anasema kuwa njia, sawa na moyo wa mwanadamu imejaa  giza. Mfano huu unatumia giza kama ishara au taashira ya mambo yasiyojulikana au yasiyoweza kutabirika.  

4) Katika uk. 61, Luka anaeleza kuwa kijiji kina mwanga kutokana na ufanisi wa  watoto wa Yona. Katika mfano huu, mwanga umetumiwa kuashiria maendeleo  yanayotokana na elimu. Baadhi ya maendeleo hayo ni watoto kupata kazi,  kuwajengea wazazi wao nyumba na kununua gari na kuenda nalo kijijini.  

5) Vilevile, mbinu ya ishara imetumika katika uk. 15 ambapo Dina anapika kwa  kuni mbichi zinazomfanya Sara kuondoka nje kwa sababu ya moshi. Kuni mbichi zinaashiria umaskini na hali ngumu ya maisha ya kijijini. Pia, ni ukosefu wa  maendeleo. Hali hii inaweza kutofautishwa na mjini ambako watu wanapika kwa kutumia jiko la gesi.  

6) Ishara pia imetumika pale ambapo tunaelezwa kuwa Salome alipata First Class  katika mtihani wake wa Chuo kikuu (uk. 28). First Class imetumika kama ishara  ya hekima na bidii masomoni.  

7) Katika uk. 33, Sara anamwambia Asna kuwa Bunju ashanunua leso yake akavaa  mpaka ikazeeka. Leso ni ishara ya zawadi au kirimu kwa mama mkwe. Hivyo  basi, Sara anamtaka Asna atafute mume amletee zawadi au amkirimu.  

Tabaini  

Ni mbinu ya fasihi ambapo jambo husisitizwa kwa kutumia kikanushi 'si'. Mbinu hii  imetumiwa na mwandishi wa Bembea ya Maisha mara kadhaa. Mifano:  

🙓 Asna: ...nyumbani pakigeuka kuwa kambi ya jeshi nitafanyaje! Amri si amri,  masharti si masharti! Asna anasisitiza hali ya ndoa anayoiona kuwa haifai.  🙓 Sara: Wewe unajua yote yaliyosemwa, hadharani na faraghani. Si makanisani, si  magengeni. Sara anasisitiza kuwa watu waliwasema kila mahali, hata  makanisani, mahali pasipofaa kusengenywa mtu. 

Tanakuzi  

Ni tamathali ya usemi inayolinganua mawazo kwa kutumia mkinzano wa maneno, virai  au sentensi kwenye miundo yenye usambamba.  

 

🙓 Katika uk. 1, Yona anasema kuwa "njaa haileti shibe". Hapa kuna mkinzano baina ya njaa na shibe.  

🙓 Katika uk. 9, Kiwa anasema kuwa dunia imekuwa ngumu kama "mwanga uletao  kivuli". Mkinzano upo baina ya mwanga na kivuli.  

MBINU ZA KIMUUNDO  

Mbinu za kimuundo hutumiwa na mwandishi kuendeleza msuko wa kazi ya fasihi.  Mwandishi wa tamthilia ya Bembea ya Maisha ametumia mbinu kadhaa za kimuundo  kujenga msuko wa tamthilia yenyewe.  

Mifano  

 Uzungumzi nafsia  

Ni aina ya monolojia itolewayo na mhusika mmoja akiwa jukwaani pekee yake. Mbinu  hii hutumiwa kuwasilisha maoni, hisia na fikra za mhusika kuhusu jambo fulani.  

🙓 Mbinu ya uzungumzi nafsia imetumika (uk. 38) ambapo Neema anazungumza  pekee yake na kudhihirisha hisia zake kuhusu maradhi yasiyosikia dawa.  Anasema maradhi hayo yanamfukarisha mtu. Mtu huwa hana la kufanya ila  kumwomba Mungu amwepushie. Ni wazi kuwa maradhi yana uzito  usiostahilimika.  

🙓 Mbinu hii pia imetumika katika (uk. 41) kwenye mazungumzo ya kibinafsi ya  Neema. Neema anajisemea kuhusu Bunju. Anasema kuwa Bunju ni zawadi  kwake kwa kuwa alimsaidia wakati alipatwa na ajali na kuwachwa katika hali  mahututi. Tunamwona pia akikumbuka maneno ya mamake kuhusu Bunju,  kuwa Bunju ni mmoja wao. Anakiri kuwa zamani hakuona hivyo kwa kuwa  mtazamo wake kuhusu mumewe ulikuwa hasi. Sasa, kwa sababu ameahidiwa  kusaidiwa kulipa gharama ya hospitalini ya Sara, mtazamo wake kuhusu Bunju  unabadilika na anmuona kama zawadi kwake.  

🙓 Uzungumzi nafsia pia unatokea katika mazungumzo ya Yona (uk. 70). Yona  anamhurumia mke wake Sara kwa sababu ya ugonjwa uliodhuru. Anasema awali aliona kuwa ni kama mzaha kuwa mkewe anaugua. Anajilaumu kuwa angejua  hangemfanyia madhila mkewe, angemtunza na Silesi za maisha wangezila  zijavyo. Tunapata nia na mwelekeo wa Yona kwa kurejelea mazungumzo yake.  Anasema ni lazima awache njia zake za awali za unywaji pombe na  kutoshughulikia familia yake. 

🙓 Mkondo anaochukuwa ni kubadilisha tabia na kuahidi kwamba siku zake za  uzeeni atazitumia kumwangalia mke wake Sara.  

Usemaji-kando  

🙓 Hii ni mbinu ambayo mhusika mmoja anasema maneno kwa hadhira au mhusika mwingine huku wenzake kwenye jukwaa wakijifanya kutosikia anachosema  mhusika huyo.  

 

🙓 Mbinu hii humsaidia msomaji kuelewa nia na kuibua msimamo wa mhusika  kuhusu mhusika mwingine, wazo au kitu fulani kinachozungumziwa katika kazi  ya fasihi kinyume na anayosema au kufanya akiwa na wahusika wengine.  Mwandishi wa tamthilia ya Bembea ya Maisha ametumia mbinu hii katika kazi  yake.  

🙓 Mbinu hii imetumika katika mazungumzo baina ya Bela na Neema (uk. 24). Bela  anaposisitiza kumwuliza Neema sababu ya kutowacha Sara alale kwake ili  wapige gumzo, Neema anageuka kando na kuuliza kwa nini Bela aendelee  kuulizia kuhusu hilo. Ni wazi kuwa Neema hataki kuzungumzia suala hilo  lihusulo mila na tamaduni. Ana hisia hasi nalo.  

🙓 Mbinu ya usemaji-kando pia imetumika katika uk. 29-30. Neema anainuka na  kuihutubia hadhira. Analalamikia hali ngumu ya maisha yanayokwenda mbio  kama gari liendalo kwa kasi. Anashangaa iwapo Bunju anamwelewa kama  ilivyokuwa hapo awali kwa kuwa hataki kumsaidia kumlipia mama yake  matibabu. Anajiuliza iwapo anaweza kumwacha mamake ateseke kwa sababu ya ugumu wa maisha.  

Mbinu rejeshi  

🙓 Mbinu rejeshi ni sehemu katika kazi ya fasihi inayozungumzia matukio katika  wakati uliopita. Pia huitwa kiangaza nyuma. Mbinu hii imetumika katika sehemu mbalimbali katika tamthilia ya Bembea ya Maisha. Kimsingi, mbinu hii  imetumika kutofautisha maisha ya jana na ya leo, kuendeleza maudhui ya  utamaduni na mabadiliko. Dina anaturejesha nyuma kiwakati katika  mazungumzo yao na Siwa ambapo anasimulia kuhusu maisha ya awali ya familia ya Yona na Sara (uk. 7). Kupitia mbinu hii, tunapata kuelewa shida ambazo Sara  na Yona walipitia, hasa masimango ya watu waliowasema kwa kukosa kupata  watoto.  

🙓 Katika (uk. 51) Bunju na Neema wanaturejesha nyuma kwenye ajali iliyompata  Neema. Bunju anasema alimpata Neema akiwa mahututi.  

🙓 Neema anakiri kuwa ilikuwa ajali mbaya sana ambayo ilisababisha vifo vingi.  Hata hivyo, Neema alinusurika baada ya kupangiwa matibabu na Bunju. Mfano  huu unaendeleza sifa ya utu na ukarimu alionao Bunju.  

🙓 Mbinu rejeshi pia imetumika katika uk. 62 kupitia mazungumzo baina ya Beni,  Luka na Yona. Hususan, Yona anakumbuka maisha yake ya awali alipokuwa  kijana na mwalimu. Yona anaeleza kuwa alikuwa anarauka kwenda shuleni,  

akiwa na kiboko mkononi na hakupenda wanafunzi kuchelewa kufika shuleni.  Vilevile, anakumbuka namna alivyovibeba vitabu kwenye baiskeli yake kwenda  kuvisahihisha wikendi. Mfano huu unadhihirisha bidii yake kabla pombe  haijamwathiri na kumbadilisha.  

🙓 Mfano mwingine wa mbinu rejeshi umetumika katika uk. 64 ambapo Neema  anakumbuka usafiri wa zamani kabla mabadiliko ya kiteknolojia. Anasema kuwa zamani wangechukua siku tatu kupambana na barabara ya vumbi, na mvua  iliponyesha, kulikuwa hakuendeki mpaka barabara ikauke ndipo safari iendelee.  Sara anachangia na kusema kuwa mwendo ulikuwa wa kobe na safari ilikuwa ya  kuchosha. Mfano huu unaendeleza maudhui ya mabadiliko ya kiteknolojia na  mgogoro baina ya jana na leo.  

Sadfa  

Sadfa katika fasihi ni hali ambapo matukio mawili hutokea kwa wakati mmoja bila  kupangwa na kwa namna ya kushangaza au inayoashiria bahati.  

Mbinu ya sadfa imetumiwa mara kadhaa katika tamthilia ya Bembeaya Maisha.  

🙓 Kwanza, mbinu ya sadfa imetumiwa katika (uk. 34) ambapo Sara na Asna  wanazungumza kuhusu ndoa ya Neema na Bunju wakiwa nyumbani kwa Asna  mjini. Ghafla, na bila kutarajiwa, Neema anaingia bila kubisha. Asna anashtuka.  

🙓 Vilevile, katika (uk. 71) Sara anamweleza Neema aende kuandaa  kiamshakinywa. Neema anaitikia wito wa mama yake na kusema kuwa ataandaa kiamshakinywa mara moja. Hata hivyo, Yona anawaeleza kuwa alikuwa  ameshaandaa tayari. Hii ni sadfa na pia kinyume cha matarajio. Neema  anaonyesha kushangazwa na kitendo hicho cha babake.  

Taharuki  

🙓 Taharuki ni hali katika kazi ya fasihi inayoibua matarajio au hali ya kutojua  kitakachofanyika hatimaye.  

🙓 Mwandishi wa tamthilia ya Bembea ya Maisha ametumia mbinu ya taharuki  kuendeleza msuko wa tamthilia yenyewe na kumpa msomaji hamu ya kusoma zaidi  kujua kitakachotokea.  

Mifano  

1) Katika onyesho la kwanza sehemu ya kwanza (uk. 1-2), mwandishi anaeleza  kuhusu ugonjwa wa Sara. Pia, Asna anaeleza kuwa Sara ataishia  

2) kumeza vidonge maisha yake yote kwa sababu ya ugonjwa huo. Kisha,  mwandishi anaonyesha Sara akisafirishwa mjini na kulazwa katika hospitali ya  bei ghali iliyo na huduma bora na wataalamu hodari kuliko hospitali za kijijini.  Mwandishi anampa msomaji hamu ya kuendelea kusoma kujua iwapo ugonjwa  wa Sara utapona.  

3) Katika uk. 10, Dina anamweleza Kiwa kuhusu namna Yona alivyoanza kulewa  kupindukia na kuanza kumpiga mkewe Sara kipigo cha mbwa. Hali hii ya Yona  na Sara pia inamulikwa kupitia kwa mazungumzo ya Asna na mamake Sara.  Msomaji anapata hamu ya kutaka kujua iwapo ulevi wa Yona ulipungua au  ulifikia kikomo.  

4) Katika uk. 28, mwandishi anadokeza kuhusu mgogoro baina ya Neema na  mumewe Bunju. Bunju anakataa kumsaidia Neema kulipia gharama ya  hospitalini kwa ajili ya matibabu ya Sara. Hata hivyo, katika  

 

5) uk. 40, Bunju anabadilisha msimamo na kuahidi kusaidia "baadaye", kisha  anaondoka. Msomaji anapata hamu ya kutaka kujua iwapo Bunju alitimiza ahadi  hiyo.  

6) Mfano mwingine wa taharuki unazuliwa na mgogoro baina ya Asna na mamake  Sara kuhusu haja ya ndoa (uk. 52-53). Asna anasema kuwa kuolewa ni hiari ya  mtu, na kuwa ndoa ni dhuluma. Kwa upande mwingine, Sara anamhimiza Asna  kutafuta mchumba aolewe amletee wajukuu na zawadi kutoka kwa mumewe.  Msomaji anapata hamu ya kujua iwapo Asna aliishia kuolewa au la.  

WAHUSIKA  

Yona  

Ni mume wa Sara na pia ni mmoja wa wahusika wakuu. Anatambulika kama mhusika  mkuu kwa sababu anahusika na takriban masuala yote yanayojadiliwa katika tamthilia  hii. Ni kama kwamba kila kitu katika tamthilia hii kinamhusu.  

Sifa zake:  

1) Mwenye bidii: Alikuwa mwalimu hodari aliyesifika kazini na udumishaji wa  nidhamu shuleni. Aliijali kazi yake na hakusita kufunga vitabu kwenye baiskeli  yake ili avisahihishe anapofika nyumbani hata siku za wikendi.  

2) Mtamaduni: Licha ya kujaliwa na mabinti waliofanikiwa maishani na kuiletea  fahari jamii yake, msukumo wa wanajamii wa kumhimiza apate mtoto wa kiume  ulimtikisa. Alikosa furaha kwenyenndoa yake kwa sababu ya kuamini mila na  desturi za jamii yake.  

3) Mwenye rabsha: Yona alipoingilia ulevi wa kupindukia alibadilika kwa njia hasi.  Alianza kumpiga mkewe hata akazirai na kumwagiliwa maji. Alishindwa  kutekeleza wajibu wake kazini na hatimaye akafutwa.  

4) Mwenye majuto: Mwishoni mwa tamthilia anajirudi na kujisuta kuhusu matatizo aliyoisababishia familia yake na hasa mke wake na kuamua kuacha kunywa  pombe.  

5) Mlevi: Yona aliposhinikizwa na wanajamii kuoa na kutafuta mtoto wa kiume  aliingilia ulevi wa kiwango cha juu.  

6) Katili: Yona ni katili na hana utu kwa sababu hata baada ya kumkuta bibi yake  akiwa katika hali mbaya ya ugonjwa, anamuuliza kwa nini hajamwandalia  chakula. Hakusaidia bibi yake katika mapishi.  

7) Ni msomi: Amesoma hadi Chuo kikuu. Alikuwa mtu wa kwanza pale kijijini  kufuzu kutoka chuoni.  

 

Umuhimu wake  

🙓 Yona anadhihirisha masaibu ya uraibu wa pombe unaoweza kuvuruga maisha ya mtu yeyote pasipo kujali nafasi yake katika jamii. Pia, anadhihirisha kwamba  vita dhidi ya uraibu wa pombe vinaweza  

🙓 shindwa ikiwa mikakati bora itatumika. Anadhihirisha ukweli wa methali kuwa  muwi huwa mwema.  

Sara  

Sara ni mke wa Yona. Yeye pia ni mhusika mkuu kwa sababu anahusika na karibu  masuala yote ya tamthilia hii. Ndoa yake ilikuwa na changamoto nyingi zikiwemo  mahitaji ya kiuchumi, fujo za mumewe ambaye alikuwa akishiriki ulevi na ugonjwa wa  moyo uliomkaba.  

 Sifa zake :  

1) Mvumilivu: Sara alivumilia mateso ya mume wake ambaye alimlaumu kwa  kutopata mtoto wa kiume. Mume wake alimtesa kutokana na kosa ambalo kwa  hakika halikuwa lake.  

2) Mpatanishi: Sara ni mpatanishi kwa kuwa alimshauri bintiye amwelewe mume  wake ambaye alitii utamaduni uliomfanya asimkubali mkwe wake alale  nyumbani kwao. Pia, alimshauri bintiye amshukuru mumewe kwa kumruhusu  kutumia hela zake kumtibu yeye aliyekuwa anaugua.  

3) Mwenye utu: Sara aliijali ndoa yake na kumpenda mumewe licha ya fujo zake.  Alikataa kukaa mjini na binti yake ili kumwepushia mume wake fedheha ya  kujifanyia kazi zilizohusishwa na wanawake kama vile kuchota maji kisimani.  

4) Mwenye hekima: Maneno anayozungumza yana wingi wa hekima na busara.  Anamweleza Asna asicheze na akili zake ijapokuwa hakupata elimu sawasawa.  5) Mlezi mwema: Anawalea wanawe kwa kuwapa mawaidha ya busara.  Anawanasihi kuheshimu ndoa, utamaduni na baba yao.  

6) Mtamaduni: Neema anatilia maanani tamaduni za jamii yake. Kwanza  tunamwona akisema kuwa fimbo hurithiwa na mtoto wa kiume. Tena  tunamwona akimtetea bwana yake kuhusiana na suala la kazi za jikoni na  kuteka maji kisimani.  

7) Mwenye uhusiano mwema: Sara alikuwa na uhusiano mwema na Dina.  Anapougua, Dina anakuja kumsaidia kwa kuwa walikuwa na uhusiano mwema.  8) Mwenye msimamo thabiti: Hata baada ya kusutwa na kukejeliwa na wanajamii  hakuyumbishwa na maneno yao. Aliwapenda mabinti zake kwa dhati. Hata  ingawa anachapwa kichapo cha mbwa na bwana yake, hakutoka nyumbani  kwake, alisimama kidete na familia yake.  

Umuhimu wake  

🙓 Sara anakuwa kielelezo chema cha wanawake walio katika ndoa zenye  misukosuko. Anavumilia na kufaulu kuwalea na kuwasomesha wanawe ingawa  mumewe anamdhulumu. 

🙓 Anaendelea kumtii mumewe na kumshauri bintiye amnasihi baba yake dhidi ya  ulevi kwa heshima.  

Neema  

Neema ambaye ni binti wa Yona na Sara ni mhusika mjenzi. Neema ni mke wa Bunju.  Wasifu wa Neema unadhihirika kutokana na kauli zake na za watu wengine pamoja na  matendo yake. Neema anadhihirisha sifa kadhaa:  

1) Mwenye bidii: Anadhihirisha mwelekeo wa mtu mwenye bidii tangu alipokuwa  shule. Licha ya kwamba wazazi wake walikuwa hawajiwezi, alisoma kwa bidii na kufaulu katika masomo yake hadi Chuo kikuu.  

2) Mwenye moyo wa kujitolea: Neema aliipenda familia yake hata alipoolewa.  Tofauti na wasichana wengine ambao hujitenga baada ya kuolewa, Neema  aliendelea kuwa nguzo imara katika familia yao. Alijitolea kumpeleka mama  yake hospitali na kugharamia ada iliyohitajika. Pia aliajiri wafanyakazi wa  kuwasaidia wazazi wake.  

3) Mwenye busara: Neema alidhihirisha busara katika ndoa yake kwa kumheshimu mumewe na kushirikiana naye katika malezi ya watoto wao tofauti na baadhi ya  wake ambao huvuruga ndoa zao kwa mivutano mambo yanapokuwa magumu.  

4) Mwenye upole. Hakujibizana na Asna dada yake wakati alikuwa akizungumza  vibaya kuhusu ndoa yake na Bunju.  

5) Amekengeuka: Neema amezinduka kwa kujua kwamba kuna tamaduni ambazo  hazifai kutiliwa maanani katika kizazi cha leo. Anamwambia Bunju kwamba  kumkataza mama yake kulala kwao ni utamaduni uliopitwa na wakati.  

6) Mwenye heshima: Neema anamheshimu baba yake hata baada ya kuwatesa  walipokuwa wachanga. Neema anamheshimu bwana yake pia. Anasema  amempa heshima yake tangu walipofunga ndoa.  

 

Umuhimu wake  

🙓 Neema anajitokeza kuwa kielelezo chema cha akina mama wenye uwezo wa  kiuchumi na kuonyesha kwamba inawezekana kudumisha amani kwenye ndoa  bila ya kusababisha ushindani usio na manufaa.  

🙓 Anadhihirisha na kuthibitisha kuwa hata mtoto wa kike anaweza kuwasaidia  wazazi wake wanapotatizika hata akiwa kwenye ndoa. Hivyo basi, anasawiriwa  kama nguzo muhimu ya kuupinga utamaduni unaomdhalilisha mtoto wa kike na  kumtukuza mtoto wa kiume.  

Asna  

Bintiye Yona wa pili. Ni mdogo wake Neema. Asna ni mhusika msaidizi. Anamsaidia  msomaji kuelewa baadhi ya masuala yanayojadiliwa katika tamthilia.  

Sifa zake:  

1) Mwenye misimamo ya kipekee: Asna anasema kwamba si lazima msichana  aolewe mara tu aingiapo utu uzima. Anaonelea kuwa watu wanastahili kupewa  nafasi ya kufanya maamuzi. Anasema taasisi ya ndoa ndiyo taasisi pekee  inayotolewa vyeti kabla ya watu kupita mtihani. Anazungumzia hali ya watu  

 

wawili wanaotoa ahadi za maisha kabla ya kufahamu ikiwa jambo  wanalojiingiza litafanikiwa au la.  

2) Mwenye heshima: Hata ingawa msimamo wake kuhusu ndoa ni tofauti na ule wa dadake, bado anamheshimu kama mkubwa wake na kuiheshimu ndoa ya Neema  ingawa anajua ina matatizo. Pia, anawaheshimu na kuwapenda wazazi wake.  

3) Amekengeuka: Asna anaelewa fika kwamba kuolewa ni kwa hiari ya mtu binafsi  ila si kushinikizwa au kulazimishwa na utamaduni.  

4) Msomi: Asna amesoma na kuhitimu hadi Chuo kikuu.  

5) Mwenye chuki: Asna anachukia tabia za Bunju za kujifanya kuwa hana pesa ilhali anazo. Anachukia ubahili.  

 

Umuhimu wake  

🙓 Asna anawakilisha vijana ambao hawana azimio la kuolewa. Wao ni sehemu ya  jamii na wanastahili kukubalika kama wale wenzao wenye imani kwenye taasisi  ya ndoa. Hata hivyo, anavyoeleza Sara, na anavyodhihirisha Neema, vijana  hawapaswi kuwa na msimamo mkali kuhusu taasisi ya ndoa kwa sababu  changamoto nyingi zilizo katika taasisi ya ndoa zinavumilika kama ilivyo katika  taasisi nyingine.  

Bunju  

Bunju ni mumewe Neema.  

Sifa zake:  

1) Mpenda haki: Bunju anamkubalia mke wake kutumia pesa zake kuishughulikia  jamii yake ambayo ina uhitaji mkubwa baada ya Yona kufutwa kazi. Pia, mama  mkwe anahitaji kutunzwa kwa hali na mali kutokana na hali yake ya kuugua kwa muda mrefu.  

2) Mwenye mapenzi: Bunju anampenda mkewe na wanawe na kutekeleza wajibu  wake wa malezi kwa bidii.  

3) Mwenye bidii: Anajitahidi kazini na mara nyingi hata muda wa kustarehe hana.  Bidii zake zinamwezesha hata kumnunulia mkewe gari.  

4) Ni mgumu wa pesa: Anajitokeza kama mwenye msimamo thabiti kuhusu  matumizi ya pesa na hivyo kusawiriwa kama mtu mchoyo au bahili.  5) Mtamaduni: Bunju anashikilia mila na desturi za jamii yake. Anapoziishi kwa  kumkataza mama mkwe kulala nyumbani kwao, anaonekana kama mtu mchoyo  na asiyejali maslahi ya mama mkwe wake. Mila na desturi zinamtawala na  kumfanya asitangamane na mama mkwe hata akiwa amelazwa hospitalini. Hili  Sio jambo jema.  

 

Umuhimu wake  

🙓 Bunju anadhihirisha umuhimu wa kushirikiana katika ndoa. Anatoa kielelezo  chema cha mume anayemjali mke wake. Ana moyo wa kusaidia.  

🙓 Alimsaidia Neema wakati alipopata ajali na kumlipia gharama zote za matibabu.  Anamsaidia Neema kwa kumruhusu atumie mshahara wake kusaidia wazazi  wake. Kwa hiyo, anampatia Neema fursa ya kusaidia jamii yake bila pingamizi.  Pia, Bunju anasimamia wanarika ambao bado wanathamini mila na desturi za  kwao kwani mwacha mila ni mtumwa.  

6. Dina  

Ni mama wa umri wa makamu na jirani wa Sara na Yona.  

Sifa zake:  

1) Mwenye moyo wa huruma: Sara anapougua, Dina anamsaidia kazi za nyumbani  na kumpa moyo kuhusu ugonjwa alionao. Anamsifu Sara kwa bidii aliyonayo  iliyomfanya kusomesha watoto wake hadi wakafikia Chuo kikuu licha ya  masimango ya wanajamii na mateso ya mumewe.  

2) Mwenye ujirani mwema: Anapoitwa na Sara amsaidie kupikia bwana yake,  anafika nyumbani mwa Sara kumsaidia katika shughuli hiyo.  

3) Mwenye roho safi: Hana kinyongo chochote kwa watoto au familia ya Sara.  Anafurahia kufanikiwa kwa watoto wa Sara.  

4) Mwenye mapenzi ya dhati: Anamsaidia rakifi yake Sara kwa dhati.  

 

Umuhimu wake  

🙓 Dina anadhihirisha usemi kwamba "Kidole kimoja hakiui chawa." Hii ni  kutokana na kujitolea kwake kumsaidia Sara kazi za nyumbani anapokuwa  anaugua. Ni kielelezo cha urafiki wa dhati na ujirani mwema. Ifahamike kwamba Sara asingeishi vyema na majirani, asingepata mtu wa kumsaidia.  

Kiwa  

Kijana wa kiume, mtoto wa Dina. Kama majirani wengine anashangazwa na bidii za  watoto wa Sara na Yona.  

Sifa zake:  

1) Mwenye heshima: Anamheshimu mama yake na kushirikiana naye licha ya pato  dogo analopata. Kupitia pato lake dogo, ameweza kubadilisha hali yao ya maisha pale nyumbani na kuinua maisha ya Dina.  

2) Mwenye roho safi: Anashangazwa na ufanisi wa majirani zake lakini hawaonei  gere.  

3) Mdadisi: Kiwa anamuuliza mama yake maswali mengi kuhusu familia ya Yona.  

 

Umuhimu wake  

🙓 Umuhimu wa Kiwa unatokana na mambo mawili; ni kijana anayewajibika na  kubadilisha maisha ya mama yake licha ya pato lake dogo. Kupitia kauli zake,  anadhihirisha kuwa ufanisi maishani hautegemei jinsia bali bidii ya mtu binafsi.  

 

Luka  

Mwanakijiji ambaye ni jirani na rafikiye Yona.  

Sifa zake:  

1) Ana busara: Anakiri kwamba siku hizi watoto wa kike wameacha kutegemea  waume zao na kuanza kuwajibikia familia zao kiuchumi.  

2) Mshauri mwema: Anamshauri Beni kuhusiana na masuala ya kitamaduni  kwamba zamani tamaduni zilikuwa lakini sasa tamaduni zingine zimepitwa na  wakati.  

Umuhimu wake  

Anadhihirisha kwamba hata vijijini mabadiliko ya kimawazo kuhusu mtoto wa kike  yameanza kukita mizizi. Anamchora Neema kama "simba wa kike" (uk. 67).  

Beni  

Mwanakijiji ambaye ni jirani na rafikiye Yona.  

Sifa zake:  

1) Mtamaduni: Anashikilia kuwa mtoto wa kiume ana manufaa kuliko wa kike.  Anadai Neema hajali maslahi ya baba yake huku akijua kuwa Neema  anamshugulikia mama yake ambaye ni mgonjwa. Hajakengeuka: Beni  hajazinduka kwa kuwa hajui tofauti kati ya injinia na fundi wa mitambo.  

2) Mchochezi: Anadai kuwa Yona anafedheheshwa kwa kuachiwa kazi za kujipikia.  Ni kama anaelekezwa na mkewe na wanawe. Ukweli ni kwamba mkewe alisafiri  mjini kwa matibabu na kukaa kwa wanawe kwa siku chache tu. Beni  anatawaliwa na taasubi ya kiume na si jirani mwema kwa Yona kwa kuwa  anachangia kumchanganya akili.  

Umuhimu wake  

🙓 Ni hasidi katika jamii. Watu wa aina hii huwachochea wenzao na mwisho  kuwatenganisha na wake na familia zao. Yona anapuuza uchochezi wa Beni na  kuonyesha kuwa sasa ameanza kupatwa na mwamko mpya.  

Bela  

Ni mfanyakazi wa nyumbani wa Neema.  

Sifa zake:  

1) Mwenye busara: Anazungumza na mwajiri wake, Neema, kuhusu matatizo  anayoyapitia kwenye ndoa yake kwa busara na kumsihi kuvumilia.  

 

2) Mtu wa kutegemewa: Ni mfanyakazi wa kutegemewa. Ana uhusiano mwema na  mwajiri wake na anaelewa kazi yake barabara. Anamkumbusha Neema kuhusu  kazi za shule za Lemi kwa maana kuwa, anaelewa jukumu lake la kuwalea  watoto wa Neema, anayeonekana kuwa mtu wa kazi nyingi.  

3) Mlezi mwema. Bela analea watoto wa Neema vizuri na kwa bidii.  

 

4) Mwenye bidii: Bela anafanya kazi ya kuwalea watoto wa Neema kwa bidii. Pia  anasema kuwa mara nyingi yeye hakupatana na watoto wake kwa sababu ya  shughuli ya kazi. Maneno hayo yanaonyesha alikuwa mwenye bidii hata kabla ya kuanza kufanya kazi kwa Neema.  

Umuhimu wake  

Anawakilisha wafanyakazi wa kiwango cha chini wanaowajibika, kuheshimu na  kuthamini kazi zao.  

Lemi  

Ni mvulana wa miaka kumi, mwanawe Bunju.  

Sifa zake:  

1) Mtiifu: Lemi anawatii wazazi wake na pia mlezi wake Bela. Anatii amri ya mama  yake anapoambiwa aende akafue hanchifu.  

2) Mwenye shukrani: Lemi anamshukuru mama yake Neema wakati alikumbushwa kufua hanchifu yake (uk. 48).  

3) Mdadisi: Lemi anauliza mama yake maswali kuhusu mama yake na bibi yake.  Lemi anauliza mama yake (uk. 30) kwa nini hana raha na maswali mengine  mengi. Pia anataka kujua ni kwa nini bibi yake hajakuja kumsalimu.  

4) Mwenye vipawa: Lemi ana kipawa cha kuimba na kucheza nyimbo kwa  miondoko na minenguo (uk. 22).  

 

Umuhimu wake  

 

Lemi anawakilisha watoto wa baadhi ya wazazi ambao hawapati wakati mwingi wa  kuingiliana na wazazi wao ambao mara mwingi wako kazini. Anawakilisha watoto  ambao hulelewa na yaya.  

Wahusika wadogo  

 

Salome na Mina: Wahusika wadogo ambao wanatajwa tu. Hawashiriki moja kwa moja  katika masuala ya tamthilia hii. Salome ni mwanawe Yona na Mina ni bintiye Bunju na  Neema.  

Umuhimu wao  

 

Wanakamilisha idadi ya watoto wa Yona na Bunju mtawalia. Idadi hii ni dhihirisho la  usasa ambapo wazazi hawapati watoto wengi kutokana na hali ibuka za kiuchumi na za  kijamii. Pia, wanaendeleza malezi ya kisasa ambapo watoto hawaonani na wazazi wao  kwa kuwa wanahudhuria masomo ya bweni au nje ya nchi.  

Ushauri muhimu kwa mtahiniwa  

 

1) Mtahiniwa sharti asome kitabu husika (Bembeaya Maisha) barabara na  kukielewa.  

2) Mwongozo ni kurunzi ya kumulikia njia, kwa hivyo, mtahiniwa sharti aelewe  aendako.  

3) Ni muhimu kusoma na kulielewa swali lililoulizwa. Ni vyema kujiuliza swali  lifuatalo: Mtahini anataka habari gani kutokana na swali hili?  

4) Usitoke nje ya muktadha wa swali na kuandaa habari ambazo hazihusiani na  swali uliloulizwa.  

5) Ikiwezekana, toa mifano kutoka kwenye tamthilia inayohusiana na jambo  unalolifafanua ili kuweka jambo hilo wazi.

 

Share On:

Support Our Website

Ads help us keep our content on kenyalivetv.co.ke free for you. Please consider supporting us by disabling your ad blocker or whitelisting our site in your ad blocker settings.

You are currently offline.
You are back online.